• HABARI MPYA

  Jumanne, Januari 22, 2019

  RONALDO AKUBALI KULIPA FAINI KESI YA KUKWEPA KODI HISPANIA

  MSHAMBULIAJI wa Klabu ya Juventus, Cristiano Ronaldo amekubali kulipa faini ya Euro milioni 18.8 sawa na shilingi bilioni 49.3 za Kitanzania kwa kosa la ukwepaji kodi nchini Hispania.
  Kwa mujibu wa hukumu iliyotolewa leo na Mahakama ya Madrid, Ronaldo amekubali pia kifungo cha miaka miwili ambacho hata hivyo hatakitumikia gerezani kutokana na utaratibu wa adhabu za vifungo nchini humo.
  Nchini Hispania hukumu ya kifungo kisichozidi miaka miwili hakipaswi kutumikiwa ndani ya gereza isipokuwa kwa kosa la uhalifu.
  Ronaldo ambaye ni mshindi mara tano wa tuzo ya mchezaji bora wa dunia alikuwa akituhumiwa kukwepa kodi kiasi cha Euro milioni 22.4 (Shilingi Bilioni 58.7) kupitia mapato yaliyotokana na matumizi ya picha zake kwenye matangazo mbalimbali kati ya mwaka 2010 na 2014 wakati akiitumikia Real Madrid.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: RONALDO AKUBALI KULIPA FAINI KESI YA KUKWEPA KODI HISPANIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top