• HABARI MPYA

    Monday, January 21, 2019

    RAJA WAPANGIWA TIMU MBILI ZA MOROCCO KOMBE LA SHIRIKISHO

    MABINGWA watetezi, Raja Club Athletic, maarufu kama Raja Casablanca wamepangwa pamoja na wapinzani wao wa Morocco, RS Berkane na Hassania Agadir kwenye Kundi A Kombe la Shirikisho Afrika.
    Katika droo iliyopangwa mjini Cairo, Misri leo ikiongozwa na mshambuliaji wa zamani wa kimataifa wa Cameroon, Patrick Mboma pamoja na Katibu Msaidizi wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Anthony Baffoe timu nyingine katika kundi hilo ni mabingwa wa Kongo, AS Otoho. 
    Kukutana kwa timu tatu za Morocco kwenye hilo, kunakumbushia michuano ya mwaka 2012, wakati timu tatu za Sudan; Al Merreikh, Al Hilal na Ahly Shendi zilipopangwa kundi moja pai, huku timu nyingine kwenye kundi lao ikiwa ni Interclube ya Angola.
    Raja Casablanca imepangwa Kundi A pamoja na RS Berkane na Hassania Agadir Kombe la Shirikisho Afrika

    Timu mbili za Tunisia, Etoile du Sahel na CS Sfaxien zimekutanishwa Kundi B pamoja na Enugu Rangers ya Nigeria na Salitas ya Burkina Faso. 
    Timu nyingine mbili za Zambia, Zesco na Nkana FC zimepangwa pamoja katika Kundi C Kombe la Shirikisho Afrika baada ya droo iliyofanyika leo makao makuu ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) mjini Cairo, Misri.
    Pamoja na Zesco na Nkana FC, klabu anayochezea beki Mtanzania, Hassan Ramadhani Kessy, timu nyingine katika kundi hilo ni Al Hilal ya Sudan na Asante Kotoko ya Ghana.
    Mabingwa mara tano Afrika, Zamalek ya Misri wamepangwa Kundi D pamoja na mabingwa wa Kenya, Gor Mahia, Petro Atletico ya Angola na NA Hussein Dey ya Algeria.

    MAKUNDI YOTE KOMBE LA SHIRIKISHO:
    Kundi A – Hassania Agadir (Morocco), AS Otoho (Kongo), RS Berkane (Morocco), Raja (Morocco)
    Kundi B – Etoile du Sahel (Tunisia), Rangers (Nigeria), Salitas (Burkina Faso), CS Sfaxien (Tunisia)
    Kundi C – Zesco (Zambia), Al Hilal (Sudan), Asante Kotoko (Ghana), Nkana (Zambia)
    Kundi D – Gor Mahia (Kenya), NA Hussein Dey (Algeria), Petro Atletico (Angola), Zamalek (Misri)
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: RAJA WAPANGIWA TIMU MBILI ZA MOROCCO KOMBE LA SHIRIKISHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top