• HABARI MPYA

  Ijumaa, Januari 25, 2019

  LUIZ AIPELEKA CHELSEA FAINALI KOMBE LA LIGI ENGLAND

  Beki Mbrazil, David Luiz akishangilia baada ya kufunga penalti ya nne ya Chelsea kuipeleka Fainali ya Kombe la Ligi England, maarufu kama Carabao Cup kufuatia ushindi wa penalti 4-2 dhidi ya Tottenham Hotspur jana Uwanja wa Stamford Bridge mjini London katika mchezo wa marudiano wa Nusu Fainali. Chelsea ilishinda 2-1 na kufanya sare ya jumla ya 2-2 kufuatia kufungwa 1-0 kwenye mchezo wa kwanza na mbali ya Luiz wengine waliofunga penalti za The Blues ni Willian, Azpilicueta na Jorginho, wakati Christian Eriksen na Erik Lamela pekee walifunga za Spurs, huku Eric Dier na Lucas Moura wakikosa. Chelsea itakutana na Manchester City katika fainali Februari 24 Uwanja wa Wembley mjini London 

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: LUIZ AIPELEKA CHELSEA FAINALI KOMBE LA LIGI ENGLAND Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top