• HABARI MPYA

  Monday, January 28, 2019

  RONALDO AFUNGA LA USHINDI JUVENTUS YAILAZA LAZIO 2-1 SERIE A

  Cristiano Ronaldo akishangilia baada ya kuifungia Juventus bao la pili kwa penalti dakika ya 88 katika ushindi wa 2-1 dhidi ya Lazio usiku wa jana kwenye mchezo wa Serie A, Italia Uwanja wa Olimpico. Emre Can alianza kujifunga dakika ya 59 kuipa Lazio bao la kuongoza, kabla ya Joao Cancelo kuisawazishia Juventus dakika ya 74. Kwa ushindi huo, Juventus inafikisha pointi 59 baada ya kucheza mechi 21, ikiendelea kuongoza Serie A kwa pointi 11 zaidi ya Napoli wanaofuatia nafasi ya pili 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: RONALDO AFUNGA LA USHINDI JUVENTUS YAILAZA LAZIO 2-1 SERIE A Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top