• HABARI MPYA

        Friday, January 18, 2019

        TUZO ZA MCHEZAJI NA KOCHA BORA WA LIGI KUU ZAPATA MDHAMINI

        Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
        SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limeitangaza kampuni ya Biko Sports kuwa Mdhamini wa tuzo za Mchezaji Bora na Kocha Bora wa mwezi wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara. 
        Biko Sports katika kipindi chote cha msimu wa 2018/2019 kilichobakia watatoa fedha kwa mchezaji bora wa mwezi na kocha bora ambapo kila mmoja atapata shilingi milioni 1.
        Mbali na fedha, Biko Sports watatoa tuzo kwa kocha na mchezaji bora wa kila mwezi.
        TFF ina utaratibu wa kuwazawadia wachezaji bora na makocha wa kila mwezi pamoja na wale wa msimu mzima. 
        • Blogger Comments
        • Facebook Comments

        0 comments:

        Item Reviewed: TUZO ZA MCHEZAJI NA KOCHA BORA WA LIGI KUU ZAPATA MDHAMINI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry