• HABARI MPYA

  Alhamisi, Januari 31, 2019

  SHIZA KICHUYA AKARIBIA KUJIUNGA NA KLABU YA LIGI DARAJA LA PILI MISRI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  WINGA wa kimataifa wa Tanzania, Shiza Ramadhani Kichuya yuko mbioni kujiunga na klabu ya Pharco ya mjini Alexandria nchini Misri.
  Taarifa ya Simba SC imesema kwamba klabu ipo kwenye mazungumzo na Pharco inayoshiriki Ligi Daraja la Pili nchini Misri ambayo yanaendelea vizuri.
  Pharco iliyoanzishwa mwaka 2010 inapigana kujaribu kupanda Ligi Kuu ya Misri na msimu huu imezidiwa kete na Al Nasr Lel Taa'en, El Sharkia na Tanta zilizofanikiwa kupanda.
  Shiza Kichuya yuko mbioni kujiunga na Pharco FC ya mjini Alexandria nchini Misri

  Kocha wa timu hiyo, Mreno Jose Rui Lopes Aguas ambaye amejiunga na timu hiyo akitokea Cape Verde, amevutiwa mno na Kichuya baada ya kuonyeshwa uwezo wake kupitia DVD.
  Na akiwa ana umri wa miaka 22, Kichuya aliyejunga na Simba SC mwaka 2016 akitokea timu ya Mtibwa Sugar ya Morogoro anapata nafasi ya kwenda kujaribu bahati yake nje.
  Tayari kuna wachezaji wawili wa Tanzania wanaocheza Ligi Kuu ya Misri ambao ni kiungo Himid Mao Mkami anayechezea Petrojet na mshambuliaji Yahya Zayd wa Ismailia, zote za Ligi Kuu na wote walikwenda huko wakitokea Azam FC. 
  Na taarifa zaidi zinaema kwamba kwa sababu Ligi Daraja la Pili Misri imemalizika kwa sasa, Pharco itamtoa kwa mkopo Kichuya klabu ya ENPPI  inayoshiriki Ligi Kuu ya nchini humo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SHIZA KICHUYA AKARIBIA KUJIUNGA NA KLABU YA LIGI DARAJA LA PILI MISRI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top