• HABARI MPYA

  Jumatano, Januari 30, 2019

  AMBOKILE WA MBEYA CITY AJIUNGA NA BLACK LEOPARDS YA AFRIKA KUSINI KWA MKOPO

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MSHAMBULIAJI wa Mbeya City, Eliud Ambokile amejiunga na klabu ya Black Leopards FC ya Ligi Kuu ya Afrika Kusini kwa mkopo wa miezi mitatu.
  Taarifa iliyotolewa na Mbeya City leo imesema kwamba Ambokile anajiunga Black Leopards FC  iliyoanzishwa mwaka 1983 katika mji wa Venda uliopo kaskazini mwa Afrika Kusini baada ya mpango wa awali wa kujiunga na El Gounah kushindikana.
  Ambokile wiki iliyopita nchini kutoka Misri baada ya wiki moja ya kufanya majaribio ya kucheza soka ya kulipwa katika klabu huyo ya Ligi Kuu ya nchini humo.

  Eliud Ambokile amejiunga na Black Leopards FC ya Afrika Kusini kwa mkopo wa miezi mitatu

  Na Mtendaji Mkuu wa Mbeya City, Emmanuel Kimbe alisema kwamba Ambokile alirejea baada ya kufanya vizuri katika majaribio yake El Gounah, lakini klabu hiyo haikufikia makubaliano na Mbeya City.
  “Hawa mabwana (El Gounah) baada ya kumjairbu kwa siku sita, wakataka kumchukua kwa mkopo, au acheze kwanza kwa miezi sita ndiyo waaamue kumnunua moja kwa moja dirisha kubwa. Lakini sisi tukaona wao kuendelea kuwa naye bila kumnunua ni kuwaminyia nafasi wengine wanaomtaka,” alisema Kimbe baada ya Ambokile kurejea kutoka Msiri.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: AMBOKILE WA MBEYA CITY AJIUNGA NA BLACK LEOPARDS YA AFRIKA KUSINI KWA MKOPO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top