• HABARI MPYA

  Jumatatu, Januari 28, 2019

  BENZEMA AFUNGA MAWILI REAL MADRID YASHINDA 4-2 LA LIGA

  Mshambuliaji Mfaransa, Karim Benzema akishangilia baada ya kuifungia mabao mawili Real Madrid dakika za nne na 45 na ushei katika ushindi wa 4-2 dhidi ya Espanyol kwenye mchezo wa La Liga jana Uwanja wa RCDE mjini Cornella de Llobregat. Mabao mengine ya Real Madrid yalifungwa na Sergio Ramos dakika ya 15 na Gareth Bale dakika ya 67, wakati ya Espanyol yamefungwa na Leo Baptistao dakika ya 25 na Roberto Rosales dakika ya 81. Pamoja na ushindi huo, Real Madrid inabaki nafasi ya tatu kwa pointi zake 39 baada ya kucheza mechi 21, nyuma ya mahasimu wao wa Jiji, Atletico Madrid wenye pointi 44, ikiendelea kuzidiwa pointi 10 na vinara, Barcelona 
      
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: BENZEMA AFUNGA MAWILI REAL MADRID YASHINDA 4-2 LA LIGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top