NDANI ya siku 10 za mwanzo wa mwezi huu (Aprili, 2015) Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limetoa ratiba mbili za michuano yake ya kimataifa, ambazo ni kufuzu Michuano ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) na Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON).
Katika CHAN, michuano ambayo hushirikisha wachezaji wanaocheza ligi za nchini mwao pekee, Tanzania itaanza na Uganda kuwania tiketi ya Fainali za Rwanda mwaka 2016.
Mechi za kwanza zitachezwa kati ya Juni 19, 20 na 21 mwaka huu na marudiano yatakuwa kati ya Julai 3, 4 na 5 mwaka 2015.
Kwa mujibu wa ratiba ya michuano hiyo iliyopangwa mjini Cairo, Misri Aprili 6, mwaka huu iwapo Tanzania itaitoa Uganda, itamenyana na Sudan iliyofuzu moja kwa moja Raundi ya Kwanza.
Katika droo hiyo iliyoongozwa na Katibu wa CAF, Hicham El Amrani aliyesaidiwa na Makamu wa Pili wa Rais wa CAF, Almamy Kabele Camara, ambaye ni Rais wa Kamati ya Maandalizi ya CHAN, Kenya itaanza na Ethiopia na Burundi itacheza na Djibouti kwa kanda ya Afrika Mashariki na Kati.
Mshindi kati ya Kenya na Ethiopia atakutana na mshindi kati ya Burundi na Djibouti katika Raundi ya Kwanza.
Mechi za kwanza za hatua hiyo zitachezwa kati ya Oktoba 16, 17 na 18 na marudiano kati ya Oktoba 23, 24 na 25 mwaka huu na washindi wa mechi hizo za Raundi ya Kwanza watafuzu moja kwa moja kwenye fainali hizo, wakiungana na wenyeji Rwanda pamoja na nchi za kanda nyingine.
Siku mbili baadaye, CAF ikatoa ratiba ya mechi za kufuzu AFCON 2017 nchini Gabon na Tanzania imepangwa Kundi G pamoja na Nigeria, Misri na Chad.
Makundi ya kufuzu AFCON 2017 kwa ujumla yapo hivi; Kundi A; Tunisia, Togo, Liberia na Djibouti. Kundi B; DRC,
Angola, Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR) na Madagascar. Kundi C; Mali, Equatorial Guinea, Benin na Sudan Kusini.
Kundi D lina timu za Burkina Faso, Uganda, Botswana na Comoros. Kundi E; Zambia Kongo, Kenya na Guinea Bissau. Kundi F, Cape Verde, Morocco, Libya na Sao Tome.
Kundi G; Nigeria, Misri, Tanzania na Chad. Kundi H; Ghana, Msumbiji, Rwanda na Mauritius. Kundi I; Ivory Coast, Sudan, Sierra Leone na Gabon. Kundi J; Algeria, Ethiopia, Lesotho na Shelisheli.
Kundi K; Senegal, Niger, Namibia na Burundi, Kundi L; Guinea, Malawi, Zimbabwe na Swaziland. Kundi M; Cameroon, Afrika Kusini, Afrika Kusini, Gambia na Mauritania.
Mara tu baada ya kutoka droo ya CHAN, Watanzania wengi wapenda soka walionyesha hali ya kukatishwa tamaa, kwamba hatuwezi kuvuka mtihani mmoja tu wa Uganda.
Hiyo inatokana na ukweli kwamba, katika kuwania tiketi ya CHAN iliyopita tulitolewa na Uganda wakitufunga nyumbani na ugenini chini ya kocha wao, Mserbia, Milutin Sredojevic ‘Micho’.
Tulifungwa 1-0 Dar es Salaam kabla ya kwenda kufungwa 3-1 Kampala na safari yetu ikaishia hapo- lakini kuelekea CHAN ya 2016 Rwanda tutaanza na Uganda tena.
Inawakatisha tamaa zaidi Watanzania kuona kwamba iwapo tutapambana na kuweza kuitoa Uganda, mbele kuna Sudan.
Wakati Watanzania bado wanatafakari kuhusu ugumu wa CHAN, CAF ikatoa na droo ya AFCON tukiwa katika kundi moja na nchi mbili mabingwa wa zamani wa michuano hiyo, Misri na Nigeria pamoja na Chad.
Hesabu za kawaida za Watanzania ziliwapa kwamba, Chad ni wepesi kwao, lakini Misri na Nigeria ni maji marefu. Tutafuzu vipi?
Lakini hiyo haipotezi ukweli juu ya kiu ya Watanania kuishuhudia tena timu yao ya taifa, ikicheza Fainali za michuano mikubwa barani.
Mara ya kwanza na ya mwisho Tanzania kucheza AFCON ni 1980, tena wakati huo bado michuano hiyo inaitwa Fainali za Kombe la Mataifa Huru Afrika.
Katika fainali hizo za Nigeria 1980, Tanzania ilitolewa raundi ya Kwanza tu, hatua ya makundi baada ya kufungwa 3-0 na Nigeria, 2-1 na Misri na kutoa sare ya 1-1 na Ivory Coast.
Mara ya kwanza na ya mwisho Tanzania kucheza CHAN ilikuwa mwaka 2009 nchini Ivory Coast tulipoishia hatua ya makundi pia.
Ili kupata tiketi ya CHAN 2009, ilibidi Tanzania izitoe Kenya, Uganda na Sudan.
Na tulifuzu bila kupoteza mechi, iwe nyumbani au ugenini, Uganda tukiwafunga 2-0 Kirumba, Mwanza na kwenda kutoa nao sare ya 1-1 Kampala, wakati Sudan tuliwafunga 3-1 Dar es Salaam na 2-1 kwao.
Lakini leo inatoka ratiba ya CHAN ya mwakani, tukiwa tumepangwa na Uganda, ambayo tukiitoa tutapambana na Sudan, Watanzania hawana ‘amani’.
Kupoteza huko kwa imani kunatokana na hali halisi ya soka ya Tanzania kwa sasa, hatuna imani nayo. Hatuna imani na timu yetu ya taifa wala wachezaji wetu.
Na japokuwa hatuna imani na timu wala wachezaji wetu, lakini mtihani unabaki pale pale, Kundi G tupo na Nigeria, Misri na Chad.
Aidha, ili kwenda fainali za AFCON Taifa Stars inapaswa kwanza kuitoa Uganda na baadaye Sudan. Hatuna imani na soka yetu kwa sababu imeporomoka na hatuna imani na timu yetu ya taifa, kwa sababu ya matokeo ya siku za karibuni mabaya.
Ni mwezi uliopita tu, tumetoka kulazimishwa sare ya 1-1 nyumbani na Malawi katika mchezo wa kirafiki, kikosini tukiwa na nyota wetu wanaocheza nje akina Mbwana Samatta, Thomas Ulimwengu na Mwinyi Kazimoto.
Na si sare tu, bali hata timu haikucheza soka ya kuvutia- kwa hivyo haistaajabishi watu kukatishwa tamaa na ratiba za CAF za kufuzu CHAN na AFCON.
Miaka mingi imepita tangu tumecheza AFCON mwaka 1980 nchini Nigeria na tayari tumekata tamaa kufuzu Fainali zijazo- je soka yetu inaelekea wapi?
Tulicheza CHAN ya kwanza mwaka 2009, baada ya hapo hatujarejea tena huko, inatoka ratiba ya kufuzu Fainali zijazo, tunajikatia tamaa, hii nini maana yake?
Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi anatakiwa kuelewa kwamba kukata tamaa ni ishara mbaya- maana yake hali ya soka yetu ni mbaya.
Tunauona mfumo mzima wa timu ya taifa kwa sasa hauleweki, kuanzia uteuzi wa wachezaji, aina ya kambi, mazoezi na hata upangaji wa timu mzaha mzaha umetawala.
Kwa kawaida timu ya taifa inapaswa kuundwa na wachezaji ambao wanacheza kwa kiwango cha juu katika wakati husika, lakini sidhani kama Mart Nooij, kocha Mholanzi wa Taifa Stars anatumia kigezo hicho.
Kwa sababu angekuwa anatumia kigezo hicho, asingemuacha kinara wa mabao Ligi Kuu katika timu yake, Simon Msuva kwenye kambi ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Malawi.
Mambo mengine kweli ni ya kitaalamu na yanategemea na falsafa za mwalimu, lakini kama zipo falsafa za kuwakataa wachezaji wanaoonyesha ubora wao uwanjani, basi hizo haziwezi kusaidia.
Wapenzi wa mpira wa Tanzania wanatazama ligi yao na wanawajua wachezaji wao bora, hivyo unavyowaundia kikosi cha timu ya taifa kisichostahili, hawawezi kukuelewa.
Nafasi ya mlinda mlango si ya kuchezea, lakini tunauona mzaha unaoendelea, wanachukuliwa makipa ambao hawadaki katika timu zao, wanaachwa wale wanaofanya vizuri. Niwe wazi zaidi hapa, kwa sasa kipa wa kwanza wa Taifa Stars anastahili kuwa Ivo Mapunda kwa sababu zote. Uwezo na uzoefu. Tafuta kipa mwingine kama huyo, utagundua Aishi Manula anainukia vizuri.
Sielewi ni siasa gani zilizotokea hata Ivo Mapunda haitwi tena Stars baada ya ujio wa Nooij.
Watanzania wenye kiu ya kuiona Taifa Stars yao inashiriki tena Fainali za mashindano makubwa, sasa wamekata tamaa baada ya droo mbili za mapema mwezi huu, CHAN na AFCON.
Huu ni ujumbe tosha kwa Rais wa TFF, Malinzi na washauri wake, kwamba Watanzania wamechoka na ngonjera zao, wanataka kuona mabadiliko, yatakayorejesha matumaini.

.png)
0 comments:
Post a Comment