• HABARI MPYA

  Alhamisi, Aprili 30, 2015

  ARSENAL YAMFUNGIA MAMA WA MCHEZAJI WAO KUFIKA UWANJANI, KISA...

  KLABU ya Arsenal imemfungia mama wa mchezaji wake wa umri wa miaka 17, winga Ainsley Maitland-Niles baada ya kumtolea 'maneno machafu' Mkuu wa majadiliano, Dick Law na kutaka kumtoa uwanjani mwanawe wakati wa mechi.
  Jule Niles alikamatwa kwa tuhuma za kutukana watu wawili katika Uwanja wa mazoezi wa klabu hiyo ya Ligi Kuu ya England mwezi Machi, kabla ya kuachiwa bila kufunguliwa mashitaka.
  Taarifa ya Telegraph Sport imesema kwamba mfanyakazi wa Uwanja wa Arsene Wenger na mtu mwingine walimshutumu mama huyo kuwatukana, wakati Law alitolewa maneno machafu alipojaribu kuingilia.
  Arsenal have banned the mother of Ainsley Maitland-Niles after she seemed to hit chief negotiator, Dick Law
  Arsenal imemfungia mama yake Ainsley Maitland-Niles baada ya kusemekana alimtukana Mkuu wa Majadiliano, Dick Law
  Maitland-Niles made his debut for Arsenal at the age of 17 years and 102 days in the Champions League
  Maitland-Niles aliichezea Arsenal katika Ligi ya Mabingwa kwa mara ya kwanza akiwa ana umri wa miaka 17 na siku 102

  Hakuna hatua zaidi zilizochukuliwa na Polisi, lakini Arsenal imemuambia mama huyo asirudi tena. Pamoja na kufungiwa, bado Niles alikwenda Uwanja wa Colney London kumuangalia mwanawe akicheza dhidi ya Aston Villa katika mecjhi ya vijana chini ya umri wa miaka 21 Ijumaa iliyopita.
  Imeelezwa Niles alitaka kuvamia uwanjani kumtoa mwanawe na Polisi wakaitwa tena na kumpa onyo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: ARSENAL YAMFUNGIA MAMA WA MCHEZAJI WAO KUFIKA UWANJANI, KISA... Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top