• HABARI MPYA

  Alhamisi, Aprili 30, 2015

  SHANGWE NA ‘VIGODORO’ MAPEMAA CHELSEA, YAIPIGA 3-1 LEICESTER, SHEREHE RASMI ZA UBINGWA JUMAPILI DARAJANI

  BADO pointi tatu Chelsea kutangaza ubingwa wa Ligi Kuu ya England msimu huu. Hiyo inafuatia ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Lecester City Uwanja wa King Power usiku wa kuamkia leo. 
  Ushindi huo umeifanya Chelsea ya kocha Mreno Jose Mourinho ifikishe pointi 80 baada ya kucheza mechi 34, mbele ya mabingwa watetezi Manchester City pointi 67 za mechi 34, Arsenal pointi 67 mechi 33 na Manchester United pointi 65 mechi 34. 
  Marc Albrighton alianza kuifungia Leicester dakika ya 54, kabla ya Didier Drogba kuisawazishia Chelsea dakika tatu baada ya kuanza kipindi cha pili.  John Terry akaifungia Chelsea zimesalia dakika 11 na Ramires akamalizia la tatu dakika ya 83.
  Chelsea inaweza kutangaza ubingwa Jumapili katika mechi na Crystal Palace Uwanja wa Stamford Bridge.
  Kikosi cha Leicester kilikuwa; Schmeichel, Wasilewski, Huth/De Laet dk24, Morgan, Albrighton, King/James dk18, Drinkwater, Cambiasso, Konchesky, Ulloa na Vardy/Mahrez dk77.
  Chelsea; Cech, Ivanovic, Cahill, Terry, Azpilicueta, Ramires, Matic, Willian/Zouma dk84, Fabregas/Mikel dk90, Hazard/Cuadrado dk88 na Drogba.
  Didier Drogba (centre) was the star of the show for Chelsea - and he was leading his team-mates in celebrations at full time
  Didier Drogba (katikati) akishangilia na wenzake jana

  PICHA ZAIDI NENDA: 

  http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-3061341/Leicester-1-3-Chelsea-Jose-Mourinho-s-one-win-away-crowned-Premier-League-champions-fighting-goal-overcome-Nigel-Pearson-s-battlers.html#ixzz3Yl7C3l29 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SHANGWE NA ‘VIGODORO’ MAPEMAA CHELSEA, YAIPIGA 3-1 LEICESTER, SHEREHE RASMI ZA UBINGWA JUMAPILI DARAJANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top