• HABARI MPYA

  Ijumaa, Aprili 24, 2015

  TIKETI ZA PAMBANO LA MAYWETAHER NA PACQUIAO SASA ZAPATIKANA KWA 'ULANGUZI'

  DAKIKA chache tu tangu kuanza kuuzwa kwa tiketi za pambano la Floyd Mayweather na Manny Pacquiao jioni ya Alhamisi, litakalofanyika ukumbi wa MGM Grand mjini Las Vegas, Mei 2 tiketi hizo zimekwisha na sasa zinapatikana kwa ulanguzi.
  Tiketi moja ilitangazwa kuuzwa kwa dola za Kimarekani 70,790 (sawa na Sh. Milioni 130,000), lakini baada ya dakika chache tu ziliisha katika mitandao halali ya mauzo na kuanza kupatikana kwa ulanguzi, tiketi moja ikiuzwa hadi dola 128,705 (Sh. Milioni 240).
  Baada ya wiki kadhaa za malumbano baina ya Mayweather Promotions na promota wa Pacquiao, Bob Arum kiasi cha tiketi 500 na 1,000 ziliingizwa sokoni Alhamisi kwa ajili ya pambano la utajiri mkubwa mwezi ujao.
  Mayweather vs Pacquiao is advertised by an escalator at the MGM Grand in Las Vegas on Wednesday
  Tiketi za pambano la Mayweather na Pacquiao zimeanza kupatikana kwa njia za panya dakika chache tu baada ya kuanza kuuzwa kihalali

  Mashabiki wa pambano walikuwa tayari kununua tiketi za 'bei poa' kupitia mgmgrand.com na ticketmaster.com ambazo siti zake gharama zake ni kuanzia dola 1,500 (Sh. Milioni 2.7), lakini na huko zimepanda hadi dola 7,500 (Sh. Milioni 13.8) kwa siti. 
  Wanunuzi wa awali walidhibitiwa kutonunua zaidi ya tiketi nne kwa mtu mmoja. baadhi ya tiketi zikiwemo zile za dola 10,000 (Sh. Milioni 18.5) hazikuingizwa sokoni na zinatarajiwa kupanda hadi dola 200,000 (karibu Sh. Milioni 400).
  MGM Grand watachukua siti 16,800 huku siti nyingine zikiwa katika mpango wa kugawanywa baina ya mapromota wa mabondia hao, kampuni mbili za Televisheni za kulipia na MGM hotel group kwa ajili ya wateja na wadau wao.
  MGM pia imetangaza mauzo ya tiketi 50,000 za kiwango cha chini kabisa, dola 100 (Sh. 185,000) kwa tiketi ambazo nazo zimepanda hadi dola 150 (Sh. 277,000), ambazo ziliingia pia sokoni Alhamisi.
  Vyombo vya habari vimetengewa siti kama 15,000 kwa mujibu wa maombi yaliyowasilishwa. Tiketi za bei poa kabisa za pambano hilo zinatarajiwa kuanza kuuzwa leo jioni katikaa ofisi za MGM Resorts kuanzia dola 10 (Sh. 18.500) kwa tiketi na mtu mmoja hataruhusiwa kununua zaidi ya tiketi 10. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: TIKETI ZA PAMBANO LA MAYWETAHER NA PACQUIAO SASA ZAPATIKANA KWA 'ULANGUZI' Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top