• HABARI MPYA

  Tuesday, April 28, 2015

  BEKI LILILOTAMBA AJAX, LIGI KUU ENGLAND NA UBELGIJI LATUA DAR KUSAKA TIMU, KAZI KWAO SIMBA, YANGA NA AZAM…

  Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
  BEKI wa zamani wa Portsmouth na Blackburn Rovers za England, Teboho Aaron Mokoena yuko nchini akitafuta timu ya kujiunga nayo kumalizia soka yake.
  Mokoena ameletwa nchini na wakala wake, Mganda Gibby Kalule ambaye ndiye amekuwa akileta wachezaji wengine hodari nchini kama Kpah Sherman wa Yanga.
  “Mokoena nipo naye hapa, maalum kwa mpango wa kujiunga na klabu moja kubwa hapa, tutaijua baadaye,”alisema Kalule.
  Mokoena mwenye umri wa miaka 34 sasa, kisoka aliibukia Jomo Cosmos ya kwao Afrika Kusini, kabla ya kwenda Bayer Leverkusen ya vijana nchini Ujerumani.
  Aaron Mokoena kulia akiwa na Gibby Kalule Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam jana wakati Yanga SC ikimenyana na Polisi Moro

  Mwaka 1999 alichukuliwa na Ajax Amsterdam ya Uholanzi alikocheza hadi mwaka 2003. Lakini katikati, 2001 na 2002 alikwenda kucheza kwa mkopo Germinal Beerschot ya Ubelgiji.
  Mwaka 2003 alichukuliwa na KRC Genk ya Ubelgiji pia aliyoichezea hadi mwaka 2005 kabla ya kuhamia England akianza kuchezea Blackburn Rovershadi mwaka 2009 aliphamia Portsmouth.
  Mwaka 2012 alirejea nyumbani Afrika Kusini ambako aliichezea Bidvest Wits hadi mwaka juzi alipopumzika.
  Mokoena aliyeichezea Bafana Bafana tangu 1999 hadi 2010 jumla ya mechi 107, sasa anataka kurejea uwanjani na ameichagua Tanzania kama sehemu ya kumrudisha kazini.
  Je, ni timu gani kati ya vigogo Simba, Yanga na Azam itafanikiwa kuinasa saini yake? Bila shaka hilo ni jambo la kusubiri na kuona.
  Mokoena anataka kumalizia soka yake Tanzania baada ya kuwika Ulaya
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BEKI LILILOTAMBA AJAX, LIGI KUU ENGLAND NA UBELGIJI LATUA DAR KUSAKA TIMU, KAZI KWAO SIMBA, YANGA NA AZAM… Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top