• HABARI MPYA

  Ijumaa, Aprili 24, 2015

  CHANONGO KUWAKOSA AZAM FC JUMAMOSI CHAMAZI

  Haroun Chanongo ni majeruhi
  Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
  AZAM FC watapata ahueni kidogo watakapokutana na Stand United Jumamosi usiku katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
  Hiyo inafuatia winga machachari wa Stand United ya Shinyanga, Haroun Athumani Chanongo kuwa majeruhi kuelekea mchezo huo.
  Mchezaji huyo wa mkopo kutoka Simba SC aliumia wakati akiichezea Stand Jumanne ikifungwa mabao 3-2 kwa mbinde na Yanga SC Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Chanongo ameshindwa kabisa kufanya mazoezi leo na wenzake kutokana na maumivu na dawati la timu hiyo iliyopanda Ligi Kuu msimu huu limesema uwezekano wa winga huyo kucheza dhidi ya Azam ni mdogo.
  Lakini bado Azam FC hawatakiwi kubweteka, kwani safu ya ushambuliaji ina wakali wengine tishio akiwemo Mnigeria Abasalim Chidiebele, mwenye mabao nane katika Ligi Kuu hadi sasa na Kheri Khalifa aliyefunga mabao yote mawili katika kipigo cha 3-2 kutoka Yanga SC.  
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: CHANONGO KUWAKOSA AZAM FC JUMAMOSI CHAMAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top