• HABARI MPYA

    Saturday, April 11, 2015

    BARCA YAPUNGUZWA KASI LA LIGA, 2-2 NA SEVILLA

    BARCELONA imevutwa jezi na kupunguzwa kasi katika La Liga, baada ya kulazimishwa sare ya 2-2 na Sevilla usiku huu Uwanja wa Ramon Sanchez Pizjuan.
    Maana yake sasa, Barca inaizidi kwa pointi mbili tu Real Madrid katika mbio za taji la La Liga, 75 kwa 73 baada ya kila timu kucheza mechi 31.
    Messi alianza kuifungia Barca dakika ya 14 kabla ya Neymar kufunga la pili dakika ya 31, lakini Sevilla ikachomoa kwa mabao ya Ever Banega dakika ya 38 na Kevin Gameiro dakika ya 84.
    Awali, Real iliichapa 3-0 Eibar, mabao ya Cristiano Ronaldo dakika ya 21, Javier Hernandez dakika ya 31 na Jese dakika ya 83.
    Neymar kulia na Messi wakishangilia baada ya kuifungia Barca leo

    PICHA ZAIDI NENDA: 

    http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-3035228/Sevilla-2-2-Barcelona-Barca-slip-Lionel-Messi-Neymar-strikes-hand-title-boost-Real-Madrid.html#ixzz3X29qnoKR 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: BARCA YAPUNGUZWA KASI LA LIGA, 2-2 NA SEVILLA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top