• HABARI MPYA

  Alhamisi, Aprili 23, 2015

  'MAFAZA' MAN CITY WAMPIGIA DEBE VIEIRA AMBADILI PELLEGRINI ETIHAD

  NAHODHA wa zamani wa Arsenal, Patrick Vieira anapigiwa debe na wachezaji wa Manchester City achukue nafasi ya kocha Manuel Pellegrini iwapo klabu itamfukuza kocha huyo aliyekalia kuti kavu.
  Mustakabali wa Pellegrini uko shakani Uwanja wa Etihad kufuatia matokeo mabaya msimu huu na Vieira anaweza kuwa miongoni mwa wanaofikiriwa kwa nafasi hiyo, iwapo bodi ya City itaamua kufanya mabadiliko.
  Na kundi kubwa la wachezaji 'mafaza' lingependa kuona Mfaransa huyo mwenye heshima kubwa Man City anapewa mikoba iwapo Pellegrini ataondoka. 
  Na kazi yake nzuri katika programu ya vijana ya klabu hiyo, inamuongezea heshima, kiasi kwamba kundi la wachezaji wakongwe linaamini Vieira anastahili kupewa nafasi ya kukinoa kikosi cha kwanza.
  Kocha chaguo la kwanza la City, Pep Guardiola bado anaendelea na kazi Bayern Munich ingawa Mkurugenzi, Txiki Beguirstain alisafiri Jumanne kwenda Ujerumani kwa ajii yaa mazungumzo naye. Hata hivyo, Guardiola ameamua kubaki Bayern angalau kwa msimu mwingine mmoja.
  Manchester City players have backed Patrick Vieira to replace Manuel Pellegrini as manager of the club - if the latter is sacked at the end of the season
  Pellegrini has endured a disappointing second season at City - and is under pressure as a result

  Wachezaji wa Manchester City wanampigia debe Patrick Vieira (kushoto) achukue nafasi ya Manuel Pellegrini Uwanja wa Etihad City's first-choice managerial option remains current Bayern Munich boss Pep Guardiola
  Kocha chaguo la kwanza Man City, Pep Guardiola ameamua kubaki Bayern Munich 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: 'MAFAZA' MAN CITY WAMPIGIA DEBE VIEIRA AMBADILI PELLEGRINI ETIHAD Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top