• HABARI MPYA

  Friday, April 24, 2015

  ADAKE NANI LEO YANGA NA RUVU, BARTHEZ AU DIDA?

  KOCHA Mholanzi, Hans van der Pluijm aliamua kumpumzisha Jumanne, kipa Ally Mustafa ‘Barthez’ baada ya kufungwa bao rahisi na Etoile du Sahel ya Tunisia wiki iliyopita.
  Deo Munishi ‘Dida’ akadaka kwa mara ya kwanza tangu Desemba 12, mwaka jana aalipofungwa mabao mawili Yanga ikilala 2-0 mbele ya masimu Simba SC katika mechi ya Nani Mtani Jembe.
  Hata hivyo, Dida aliyekuwa kipa namba moja mwaka jana Jangwani, naye aliruhusu mabao mawili Yanga ikishinda 3-2 katika mfululizo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
  Deo Munishi 'Dida' alifugwa mabao mawili na Stand United Jumanne
  Ally Mustafa 'Barthez' (kushoto) alipumzishwa baada ya kufungwa bao la rahisi na Etoile 

  Wakati leo Yanga SC inaikaribisha Ruvu Shooting ya Pwani Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kusaka pointi tatu kati ya sita inazohitaji kutangazwa ubingwa- bila shaka nani atadaka ni vigumu kujua.  
  Wazi sasa Mholanzi, Pluijm kichwa kitakuwa kinamuuma kuhusu makipa wake, na haitakuwa ajabu Barthez aliyefungwa bao rahisi katika mchezo wa kwanza hatua ya 16 Bora Kombe la Shirikisho akarejea langoni leo.   
  Barthez alifungwa bao hilo mapema tu kipindi cha pili, wakati huo Yanga inaongoza 1-0, inawezekana alikuwa ‘hajakaa sawa’ na mfungaji alimsoma.
  Lakini mabao mawili aliyoruhusu Dida Jumanne, wazi yanamuweka katika wakati mgumu kurejea langoni leo.
  Na inawezekana pia kutopata mechi kwa muda mrefu kulichangia Dida kufungwa mabao hayo mwanzoni mwa wiki na kama ataendelea kudaka mechi kadhaa, atarudi katika ubora wake.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ADAKE NANI LEO YANGA NA RUVU, BARTHEZ AU DIDA? Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top