• HABARI MPYA

  Monday, April 27, 2015

  HAZARD MWANASOKA BORA ENGLAND, KANE MWANASOKA BORA CHIPUKIZI

  WASHINDI WOTE WA TUZO ZA PFA 2015 

  Mchezaji Bora wa Kike wa PFA: Ji So-yun
  Mchezaji Bora Chipukizi wa Kike wa PFA;: Leah Williamson
  KIUNGO wa Chelsea, Eden Hazard ameendelea kung'ara katika soka ya Uingereza baada ya kuteuliwa Mwanasoka Bora wa Mwaka wa Chama cha Wachezaji wa Kulipwa England (PFA).
  Mchezaji huyo nyota wa Ubelgiji mwenye umri wa miaka 24, ameifungia Chelsea mabao 18 katika mashindano yote msimu huu, akiiwezesha kutwaa taji la Kombe la Ligi maarufu kama Capital One na kuwasogeza karibu kabisa na ubingwa wa Ligi Kuu kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2010.
  Alipewa tuzo hizo kutokana na soka yake 'babu kubwa' katika ukumbi wa hoteli ya Grosvenor mjini London usiku wa kuamkia leo.
  Ushindi katika mechi mbili zjijazo za Chelsea dhidi ya Leicester na Crystal Palace nyumbani Uwanja wa Stamford Bridge utaifanya Chelsea ijihakikishie ubingwa ligi ikiwa inaendelea.
  Eden Hazard poses with the PFA trophy after winning the award with a superb season in a Chelsea shirt
  Eden Hazard akiwa na tuzo yake ya PFA usiku wa kuamkia leo London

  PICHA ZAIDI NENDA: 
  http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-3056557/Eden-Hazard-wins-PFA-Player-Year-award-following-stellar-season-champions-elect-Chelsea.html#ixzz3YTkHuPJ2 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: HAZARD MWANASOKA BORA ENGLAND, KANE MWANASOKA BORA CHIPUKIZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top