• HABARI MPYA

  Thursday, April 23, 2015

  YANGA SC KUMKOSA MBUYU TWITE KESHO DHIDI YA RUVU SHOOTING TAIFA, TELELA NA CANNAVARO NAO ‘BADO BADO’

  Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
  YANGA SC itamkosa kiraka wake, Mbuyu Twite katika mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Ruvu Shooting Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kwa sababu atakuwa anatumikia adhabu ya kadi tatu za njano.
  Pamoja na hayo, vinara hao wa Ligi Kuu, wataendelea kukosa huduma ya Nahodha wao, Nadir Haroub Ali ‘Cannavaro’ aliyeumia katika mechi dhidi ya Etoile du Sahel wiki iliyopita Uwanja wa Taifa.
  Cannavaro hakurejea uwanjani baada ya dakika 45 za kwanza za mchezo huo wa kwanza hatua ya 16 Bora Kombe la Shirikisho Afrika, baada ya kuumia, timu hizo zikitoka sare ya kufungana bao 1-1.  
  Mbuyu Twite (kushoto) na Cannavaro (kulia) wote watakosekana kesho

  Aidha, kiungo tegemeo wa timu hiyo, Salum Abdul Telela ‘Master’ aliyeumia wiki mbili zilizopita katika mchezo dhidi ya Kagera Sugar, naye ataendelea kukosekana kesho.
  Yanga SC inahitaji pointi zote sita katika mechi zake mbili zijazo kuanzia kesho ili kujihakikishia ubingwa wa Ligi Kuu, kwani itafikisha pointi 55 ambazo haziwezi kufikiwa na wapinzani wao, Azam FC ambao pia ni mabingwa watetezi. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA SC KUMKOSA MBUYU TWITE KESHO DHIDI YA RUVU SHOOTING TAIFA, TELELA NA CANNAVARO NAO ‘BADO BADO’ Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top