• HABARI MPYA

    Wednesday, April 22, 2015

    CHICHARITO AIPELEKA REAL MADRID NUSU FAINALI LIGI YA MABINGWA

    BAO pekee la Javier Hernandez ‘Chicharito’ usiku huu Uwanja wa Bernabeu, limeipa ushindi wa 1-0 Real Madrid katika Robo Fainali ya pili ya Ligi ya Mabingwa, dhidi ya mahasimu, Atletico Madrid.
    Real sasa inakwenda Nusu Fainali ya michuano hiyo kwa ushindi wa jumla wa 1-0 baada ya sare ya 0-0 katika mchezo wa kwanza. Real inasonga mbele, siku moja baada ya mahasimu wao wakubwa Hispania, Barcelona nao kuitoa PSG na kutinga hatua hiyo.   
    Mshambuliaji wa mkopo kutoka Manchester United, Chicharito alifunga dakika ya 88, likiwa bao lake la kwanza katika Ligi ya Mabingwa ndani ya siku 895.
    Atletico Madrid ilipata pigo dakika ya 76, baada ya kumpoteza nyota wake, Arda Turan aliyetolewa kwa kadi ya pili ya njano baada ya kumchezea rafu Sergio Ramos.
    Kikosi cha Real Madrid kilikuwa; Casillas, Carvajal, Pepe, Varane, Coentrao, Ramos, Kroos, Isco, Rodriguez, Hernandez na Ronaldo.
    Atletico Madrid; Oblak, Juanfran, Miranda, Godin, Gamez, Turan, Tiago, Koke, Saul/Gabi dk46, Griezmann/Raul Garcia dk65 na Mandzukic. 
    Javier Hernandez 'Chicharito' akishangilia baada ya kuifungia bao pekee Real Madrid dakika za lala salama katika Robo Fainali ya pili ya Ligi ya Mabingwa

    PICHA ZAIDI NENDA: 
    http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-3051041/Real-Madrid-1-0-Atletico-Madrid-agg-1-0-Javier-Hernandez-settles-derby-book-place-Champions-League-semi-finals-Arda-Turan-sent-visitors-Bernabeu.html#ixzz3Y4dnyzGD
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: CHICHARITO AIPELEKA REAL MADRID NUSU FAINALI LIGI YA MABINGWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top