• HABARI MPYA

  Jumatano, Aprili 29, 2015

  YANGA SC; NDIYE BABA LAO LIGI KUU, WENGINE WATASUBIRI SANA

  Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
  MAPEMA wiki hii, Yanga SC iliendelea kuvunja rekodi yake- baada ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kwa mara ya 25.
  Yanga SC imetwaa ubingwa wa Ligi Kuu ikiwa ina mechi mbili mkononi- baada ya kufikisha pointi 55 ambazo haziwezi kufikiwa na waliokuwa mabingwa watetezi, Azam FC.
  Yanga SC ndiyo klabu iliyotwaa mara nyingi zaidi ubingwa wa Bara, 25 ikifuatiwa na mahasimu wao, Simba SC mara 18, Mtibwa Sugar mara mbili, Cosmopolitans mara moja sawa na Mseto (sasa haipo), Pan Africans, Tukuyu Stars, Coastal Union na Azam FC.
  Simba SC ndiyo mabingwa wa kwanza wa Ligi Kuu, mwaka 1965 wakati huo bado wanajulikana kama Sundeland na wakafanikiwa kutetea taji hilo mwaka uliofuata, kabla ya kupokonywa na Cosmospolitan mwaka 1967. 
  Yanga SC walilitwaa taji mara ya kwanza kabisa mwaka 1968 na wakalitetea kwa miaka minne mfululizo. Endelea.

  ORODHA YA MABINGWA WA LIGI KUU BARA
  1965 - Sunderland (sasa Simba, Dar es Salaam)
  1966 - Sunderland (Dar es Salaam)
  1967 - Cosmopolitans (Dar es Salaam)
  1968 - Young Africans (au Yanga, Dar es Salaam)
  1969 - Young Africans (Dar es Salaam)
  1970 - Young Africans (Dar es Salaam)
  1971 - Young Africans (Dar es Salaam)
  1972 - Young Africans (Dar es Salaam)
  1973 - Simba (Dar es Salaam)          
  1974 - Young Africans (Dar es Salaam)
  1975 - Mseto Sports (Morogoro)  
  1976 - Simba (Dar es Salaam)
  1977 - Simba (Dar es Salaam)
  1978 - Simba (Dar es Salaam)
  1979 - Simba (Dar es Salaam)
  1980 - Simba (Dar es Salaam)
  1981 - Young Africans (Dar es Salaam)         
  1982 - Pan African (Dar es Salaam)
  1983 - Young Africans (Dar es Salaam)
  1984 - Simba (Dar es Salaam)
  1985 - Young Africans (Dar es Salaam)
  1986 - Tukuyu Stars (Mbeya)
  1987 - Young Africans (Dar es Salaam)
  1988 - Coastal Union (Tanga)
  1989 - Young Africans  (Dar es Salaam)
  1990 – Simba (Dar es Salaam)
  1991 - Young Africans (Dar es Salaam)
  1992 - Young Africans (Dar es Salaam)
  1993 - Young Africans (Dar es Salaam)
  1994 - Simba (Dar es Salaam)
  1995 - Simba (Dar es Salaam)
  1996 - Young Africans (Dar es Salaam)
  1997 - Young Africans (Dar es Salaam)
  1998 - Young Africans (Dar es Salaam)
  1999 – Mtibwa Sugar (Morogoro)
  2000 – Mtibwa Sugar (Morogoro)
  2001 - Simba  (Dar es Salaam)
  2002 - Young Africans (Dar es Salaam)
  2003 – Simba (Dar es Salaam)
  2004 - Simba (Dar es Salaam)
  2005 - Young Africans (Dar es Salaam)
  2006 - Young Africans (Dar es Salaam)
  2007 - Simba (Dar es Salaam) 
  2008 - Young Africans (Dar es Salaam)
  2009 - Young Africans (Dar es Salaam)
  2010 - Simba (Dar es Salaam)
  2011 - Young Africans (Dar es Salaam)
  2012 - Simba (Dar es Salaam)
  2013 - Young Africans (Dar es Salaam)
  2014 - Azam FC (Dar es Salaam)
  2015 –Yanga SC (Dar es Salaam) 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: YANGA SC; NDIYE BABA LAO LIGI KUU, WENGINE WATASUBIRI SANA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top