• HABARI MPYA

    Alhamisi, Aprili 30, 2015

    ARSHAVIN WA ARSENAL 'AFUNGASHIWA VIRAGO' URUSI

    MSHAMBULIAJI wa zamani wa Arsenal, Andrei Arshavin atatemwa na vinara wa Urusi, Zenit St Petersburg mwishoni mwa msimu, sambamba na kiungo mkongwe wa Ukraine, Anatoly Tymoshchuk.
    Kocha wa Zenit, Andre Villas-Boas amesema klabu haijafanya mazungumzo ya kuongeza Mkataba na wawili hao, ambao mikataba yao ya sasa inamalizika mwishoni mwa msimu.
    Kocha huyo wa zamani wa Chelsea na Tottenham amesema mikataba ya wachezaji hao inamalizika na hakuna mazungumzo yaliyofanyika hadi sasa kwa ajili ya mikataba mipya.
    Andrei Arshavin is set to leave Russian side Zenit St Petersburg when his contract expires in the summer
    Andrei Arshavin anatarajiwa kuondoka Zenit St Petersburg Mkataba wake utakapomalizika

    Arshavin, mwenye umri wa miaka 33 sasa, ambaye amechezea The Gunners kuanzia mwaka 2009 hadi 2013, anaichezea kwa mara ya tatu Zenit na zaidi amekuwa akiingia kutokea benchi katika mechi 17 msimu huu.
    Nahodha wa Ukraine, Tymoshchuk, mwenye umri wa miaka 36 sasa, alijiunga na klabu hiyo mwaka 2013 baada ya kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa na Bayern Munich na msimu huu amecheza mechi 21.
    Zenit kwa sasa inaongoza Ligi Kuu Urusi kwa pointi zaidi dhidi ya Krasnodar wanaowafuatia.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 maoni:

    Item Reviewed: ARSHAVIN WA ARSENAL 'AFUNGASHIWA VIRAGO' URUSI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top