• HABARI MPYA

  Jumatano, Aprili 29, 2015

  ANDER HERRERA MCHEZAJI BORA MPYA MAN UNITED, PAUL SCHOLES HUYO

  KIUNGO wa zamani wa kimataifa wa England, Paul Scholes amesema Ander Herrera ndiyo usajili bora wa msimu Manchester United.
  Mspanyola huyo, Herrera amekuwa katika kiwango kizuri Manchester United na amevutia zaidi mzunguko wa pili wa LIgi Kuu England Uwanja wa Old Trafford.
  Herrera alisotea nafasi kwenye kikosi cha Mholanzi Louis van Gaal katika miezi yake ya mwanzoni baada ya kutua Ligi Kuu ya England, lakini sasa amekuwa 'lulu'.
  Ander Herrera has been a stand-out star for Manchester United and has now won praise from Paul Scholes
  Ander Herrera amemvutia gwiji wa Manchester United, Paul Scholes
  Scholes said that while Herrera struggled in the early months of his United career, he is now looking better
  Scholes amesema Herrera ndiyo usajili bora wa msimu Manchester United

  Na wakati klabu ilisajili wachezaji wenye majina makubwa kama Radamel Falcao na Angel di Maria ambao wameshindwa kukidhi matarajio, Scholes amesema kiungo aliyesajiliwa kwa Pauni Milioni 29, Herrera ndiye bora kwa msimu kati ya wachezaji walionunuliwa na kocha huyo Mholanzi.
  "Nafikiri ilikuwa vigumu kwa wachezaji wote wapya mwanzoni. Miezi sita, saba, nane ya mwanzo ilikuwa migumu. Herrera amekuwa mmoja aliyevutia zaidi. Alikuwa mchezaji mwingine aliyesitea namba kikosi cha kwanza mwanzoni, lakini sasa anachea visuri mno, mpira mzuri haswa," amesema gwiji huyo wa Manchester United.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: ANDER HERRERA MCHEZAJI BORA MPYA MAN UNITED, PAUL SCHOLES HUYO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top