• HABARI MPYA

  Alhamisi, Aprili 23, 2015

  KOPUNOVIC AWATANGAZIA VITA RASMI AZAM FC, ASEMA; “NAFASI YA PILI TUNAITAKA KWELI”

  Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
  KOCHA wa Simba SC, Mserbia Goran Kopunovic amesema kwamba ushindi wa jana wa mabao 4-0 dhidi ya Mgambo JKT umeamsha matumaini mapya ya kumaliza katika nafasi ya pili kwenye Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
  Na Mserbia huyo amesema kwamba sasa wanapambana waweze kushinda mechi zao zote zilizobaki ili wapate nafasi hiyo ya pili, wanayoishindania dhidi ya mabingwa watetezi, Azam FC.
  Mshambuliaji Mganda, Emmanuel Okwi jana amepiga ‘hat-trick’ Simba SC ikiibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya JKT Mgambo Shooting katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, bao lingine akifungaa mzalendo Ramadhani Singano ‘Messi’.
  Nafasi ya pili; Kocha wa Simba SC, Goran Kopunovic amesema wanaitaka nafasi ya pili Ligi Kuu

  Ushindi huo, umewafanya Wekundu wa Msimbazi watimize pointi 38 baada ya kucheza mechi 23, wakiendelea kukaa nafasi ya tatu nyuma ya Azam FC yenye pointi 42 za mechi 22. 
  Timu mbili za mbili katika Ligi Kuu hucheza michuano ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF), bingwa akicheza Ligi ya Mabingwa na mshindi wa pili Kombe la Shirikisho.
  Yanga SC wapo kileleni kwa pointi zao 49 za mechi 22 na wanahitaji pointi sita zaidi ili kujihakikishia ubingwa.
  Akizungumza jana baada ya mechi na Mgambo, kocha wa zamani wa Polisi ya Rwanda alisema; “Nawapongeza vijana wangu kwa kucheza vizuri, tunaendelea kupambana katika kuifukuzia nafasi ya pili. Kimahesabu bado nafasi tunayo, sasa tunakwenda kujiandaa na mechi ijayo dhidi ya Ndanda,”alisema Kopunovic.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: KOPUNOVIC AWATANGAZIA VITA RASMI AZAM FC, ASEMA; “NAFASI YA PILI TUNAITAKA KWELI” Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top