• HABARI MPYA

  Jumanne, Aprili 28, 2015

  PAMOJA NA KUBEBA UBINGWA LIGI KUU, YANGA SC HATARINI KUTOSHIRIKI LIGI YA MABINGWA AFRIKA, NA AZAM INAWAHUSU PIA

  Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
  YANGA SC jana wamejihakikishia ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, lakini kuna hatari mwakani wasicheza Ligi ya Mabingwa Afrika.
  Azam FC inakwenda vizuri katika mbio za kuwania nafasi ya pili, ikikabiliwa na upinzani wa Simba SC- nafasi ambayo hutoa mwakilishi wan chi katika michano ya Kombe la Shirikisho Afrika.
  Timu za Tanzania zinakabiliwa na hatari ya kuenguliwa kwenye michuano ya Afrika kutokana na sheria mpya ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF)  ya leseni za klabu.
  Rais wa TFF, Jamal Malinzi amesema jana mjini Dar es Salaam kwamba, iwapo klabu hazitajaza fomu za leseni za klabu zilizotolewa na CAF, basi mwakani hazitashiriki michuano ya Afrika.
  Mabingwa wapya wa Tanzania Bara, Yanga SC wanaweza kukosa michuano ya Ligi ya Mabingwa mwakani

  Malinzi amezikumbusha klabu nchini kujaza fomu walizopewa za leseni za klabu ili kujiepusha na hatari ya kukosa kushiriki michuano hiyo.
  “Napenda nitumie fursa hii, kuwakumbusha klabu kwamba, wanatakiwa kujaza fomu za leseni za klabu, vinginevyo wajue kuna hatari ya kutocheza michuano ya Afrika,”amesema Malinzi.
  Naye Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya CAF, Leodegar Tenga amesistiza juu ya hilo akizitaka klabu kutofanya mzaha katika hilo.
  “Suala la leseni za klabu ni muhimu mno, lazima klabu zetu zijaze leseni hizo ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kuendelea kucheza michuano ya Afrika,”amesema jana Tenga, Rais wa zamani wa TFF na Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA).      
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: PAMOJA NA KUBEBA UBINGWA LIGI KUU, YANGA SC HATARINI KUTOSHIRIKI LIGI YA MABINGWA AFRIKA, NA AZAM INAWAHUSU PIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top