• HABARI MPYA

  Ijumaa, Aprili 24, 2015

  GUARDIOLA AANZA MIKAKATI YA KUMZUIA MESSI, ASEMA...

  KOCHA Pep Guardiola amesema kwamba sasa anatakiwa kuanza kutafuta mbinu za kumzuia mshambuliaji Lionel Messi.
  Akiwa anaelekea kukutana na mchezaji mkubwa katika historia ya Barcelona, Guardiola – kocha mkubwa katika historia ya klabu hiyo amesema; "Tutaona namna gani tunaweza kufanya katika kila moja ya mechi hizo mbili na tutajaribu kutengeneza mfumo mzuri wa uzuiaji utakaomzuia Messi,". "Ni timu ya ajabu, lakini nasi tupo hivyo.'
  Guardiola nurtured Messi into the best player in the world while manager at the Nou Camp
  Guardiola akimpa maelekezo Messi wakati alipokuwa kocha Nou Camp

  Guardiola anarejea Barcelona katika timu ambayo sasa inafundishwa na Luis Enrique ambayo bado inacheza soka nzuri tangu aondoke mwaka 2013.
  "Itakuwa mechi maalum sana kwangu"amesema baada ya kupangwa na Barcelona katika Nusu Fainali za Ligi ya Mabingwa Ulaya leo. 
  "Itakuwa mechi maalum pia kwa Thiago (Alcantara) na kwa watu wengine wa benchi la ufundi. Nimeishi maisha yangu yote Barcelona, ni nyumbani kwangu,".
  Guardiola alidhihirisha mapenzi yake kwa klabu hiyo baada ya kwenda na baba yake kuishuhudia Barca ikiifunga Manchester City katika hatua ya 16 Bora akiwa jukwaani Uwanja wa Camp Nou.
  Alijitahidi kuficha namna anavyomkubal Messi usiku huo, lakini bado akanaswa na kamera akishangilia vitu vya mshindi huyo wa Balon d'Or nne.
  Na amesema Messi anaweza kuiadhibu Bayern ikiwa watacheza kizembe kama walivyofanya katika Robo Fainali ya kwanza dhidi ya Porto. "Ikiwa tutafanya makosa kama tuliyofanya katika mechi hiyo, tutakwisha kwa Barcelona," amesema.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: GUARDIOLA AANZA MIKAKATI YA KUMZUIA MESSI, ASEMA... Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top