• HABARI MPYA

    Tuesday, April 28, 2015

    FERGUSON: RONALDO ANAWEZA KUNG'ARA POPOTE, HATA MILLWAL, QPR... MESSI NI WA BARCELONA TU

    KOCHA wa zamani wa Manchester United, Sir Alex Ferguson ametaja sababu za wakati wote kumuona Cristiano Ronaldo yuko juu ya Lionel Messi wakati anazungumza na John Parrott wakicheza pool table, maarufu pia kama snooker.
    Kocha huyo mwenye mafanikio makubwa zaidi katika historia ya soka ya Uingereza amezungumza na Parrott na mtangazaji Hazel Irvine katika mahojiano maalum ya BBC ya michuano ya Ubingwa wa Dunia Crucible.
    Ferguson amesema wakati wote anaulizwa nani ni mchezaji bora duniani?, kabla ya kufafanua kwa nini humchagua mchezaji wake wa zamani United dhidi ya nyota wa Barcelona.
    Former Manchester United amanger Sir Alex Ferguson (left) speaks with John Parrott over a frame of snooker
    Kocha wa zamani wa Manchester United, Sir Alex Ferguson (kushoto) akizungumza na John Parrott kwenye meza ya snooker

    Ferguson anaamini Cristiano Ronaldo ni mzuri zaidi ya Lionel Messi kwa sababu anaweza kufunga akiwa na timu yoyote

    "Watu wengi kwa urahisi tu wanasema Messi na huwezi kukataa maoni yao,"alimuambia bingwa wa mwaka 1991 wa Snooker duniani.
    "Ronaldo anaweza kuchezea Millwall, QPR, Doncaster Rovers, (timu moja) yoyote, na akafunga hat-trick. Sina uhakika kama Messi anaweza kufanya hivyo. Ronaldo yuko fiti mno, ana kasi, mzuri wa kurukia mipira ya juu kupiga kichwa na mkali.
    "Nafikiri Messi ni mchezaji wa Barcelona,' amesema.
    Kocha huyo wa zamani wa United wakati wote amekuwa na uhusiano mzuri na nyota huyo anayecheza Real Madrid kwa sasa tangu aondoke Old Trafford, na Ferguson anampa heshima Mreno huyo sambamba na Ryan Giggs na Paul Scholes kama wachezaji bora duniani aliowahi kuwafundisha.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: FERGUSON: RONALDO ANAWEZA KUNG'ARA POPOTE, HATA MILLWAL, QPR... MESSI NI WA BARCELONA TU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top