• HABARI MPYA

  Jumatatu, Aprili 27, 2015

  DIDDY NA 'MSHKAJI' WAKE MARK WAHLBERG WAWEKA MILIONI 500 MAYWEATHER ATAMPIGA PACQUIAO

  MWANAMUZIKI Sean Combs 'Diddy' ameweka dau la dola za Kimarekani 100,000 (Sh. Milioni 200) kumtabiria Floyd Mayweather ushindi dhidi ya Manny Pacquiao.
  Mabondia hao watapigana Mei 2, mwaka huu ukumbi wa MGM Grand Casino katika pambano la kumaliza ubishi nani mkali baina yao.
  Na rapa huyo ambaye pia ni prodyuza ameweka dau la dola 250,000 (Milioni 500) kwa pamoja na mwigizaji wa Hollywood na rafiki yake, Mark Wahlberg kwamba ‘Money’ Mayweather atashinda pambano.
  Katika video waliyoposti Instagram, Diddy awali aliweka dau la dola 100,000, kabla ya Wahlberg kuongezea wakati wawili hao wakiwa wameketi wanazungumza katika eneo la bwawa la kuogelea.
  Diddy and Mark Wahlberg placed a bet of $250,000 on Floyd Mayweather and Manny Pacquiao mega-fight
  Diddy na Mark Wahlberg wameweka dola 250,000 kumtabiria Floyd Mayweather atampiga Manny Pacquiao

  Lakini Diddy na Wahlberg si pekee waliopanga kuweka dau kutabiri mshindi kuelekea pambano hilo litakalofanyika Las Vegas, ambalo dau lake linatarajiwa kupanda hadi dola Milioni 400.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: DIDDY NA 'MSHKAJI' WAKE MARK WAHLBERG WAWEKA MILIONI 500 MAYWEATHER ATAMPIGA PACQUIAO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top