• HABARI MPYA

  Tuesday, April 28, 2015

  PACQUIAO: NATAKA KUMTANDIKA KAMA BEGI MAYWEATHER, KILA RAUNDI NAMCHAPA MIMI TU

  Pacquiao akielekea Las Vegas
  BONDIA Manny Pacquiao amehamishia kambi yake katika hoteli ya Mandalay Bay mjini in Las Vegas kwa maandalizi ya mwisho kuelekea pambano lake la kumaliza ubishi Jumamosi dhidi ya Floyd Mayweather ukumbi wa MGM Grand mjini Los Angeles.
  Pacquiao ameondoka jana kwenye kambi yake ya mazoezi LA alipokuwa amefikia katika hoteli yake ya kawaida, Vegas kwenda kufanya maandalizi ya mwisho huku akisema hatarajii kumpiga Mayweather kwa Knockout (KO).
  Mashabiki walijitokeza na kulizunguka kwa wingi LA basi la bondia huyo wa Ufilipino kumuaga wakati wanaondoka nje ya klabu ya Wild Card Boxing, Las Vegas. 
  Pacquiao gets in his last workout in Los Angeles before heading to Las Vegas and the Mandalay Bay Hotel on Monday
  Pacquiao ameondoka Los Angeles na kwenda kuweka kambi Las Vegas katika hoteli ya Mandalay Bay jana

  Basi hilo lenye siti 54 kali ni kubwa lenye uwezo wa kubeba watu wengi, ambalo ndani yake pamoja na Pacquiao mwenyewe, alikuwepo mkewe, Jinkee kwa safari hiyo ya maili 276 kuelekea Vegas.
  Wakati akijiandaa na safari hiyo, mbabe huyo wa Ufilipino aliwastaajabisha wengi baada ya kusema hatarajii kumshinda mpinzani wake kwa Knock-out (KO) Jumamosi, na kwamba anataka kushinda kila raundi dhidi ya Mayweather ambaye hajawahi kupoteza pambano.
  "Kabisa sitafuti knock-out," amesema Pacquiao. "Hatutafuti knock-out tu, lakini ni kurusha ngumi nyingi, na pia kuhakikisha kwamba kila raundi tunaongoza pointi," amesema.
  Kocha wake, Freddie Roach amemuunga mkono bondia wake, akisema; "Unaweza kumpiga Floyd Mayweather ikiwa utamhenyesha na kumnyima nafasi ya kufanya mambo yaliyomfanya atambe,:.
  "Manny ana ngumi nzito haswa, lakini nataka amzidi kwa kurusha ngumi (Mayweather) katika kila raundi. Nafikiri tunaweza kushinda baada ya raundi zote 12. Tunataka kutupa ngumi kibao,"A tour bus carrying guests and members of Pacquiao's training camp, displaying his face, leaves for Las Vegas on Monday

  Basi la kitalii lilobeba timu ya Pacquiao likiwa limepambwa picha ya bondia huyo kuelekea Las Vegas jana

  PICHA ZAIDI NENDA: 

  http://www.dailymail.co.uk/sport/boxing/article-3058354/Manny-Pacquiao-gets-final-training-Los-Angeles-heads-Las-Vegas-hotel-ahead-Floyd-Mayweather-fight.html#ixzz3YZRDcScn 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: PACQUIAO: NATAKA KUMTANDIKA KAMA BEGI MAYWEATHER, KILA RAUNDI NAMCHAPA MIMI TU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top