• HABARI MPYA

  Jumatano, Aprili 29, 2015

  NIYONZIMA AACHWA YANGA SC SAFARI YA TUNISIA, NGONYANI ‘AFUNGA MKANDA’ ANGANI

  Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
  YANGA SC imeondoka usiku huu kwenda Tunisia kwa ajili ya mchezo wa marudaino hatua ya 16 Bora Kombe la Shirikisho Afrika bila kiungo wake hodari na tegemo, Haruna Hakizimana Fadhil Niyonzima ambaye ni majeruhi.
  Imeshindikana Niyonzima kwenda kuisaidia Yanga SC katika mchezo huo muhimu- kutokana na kuwa bado hajapona.
  Wachezaji walioondoka na Yanga SC usiku huu ni makipa; Ally Mustafa ‘Barthez’ na Deo Munishi ‘Dida’, mabeki Pato Ngonyani, Oscar Joshua, Edward Charles, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, ’Juma Abdul, Rajab Zahir, Mbuyu Twite na Kevin Yondan.
  Haruna Niyonzima kushoto amekosa safari ya Tunisia 

  Viungo ni Nizar Khalfan, Andrey Coutinho, Salum Telela na Said Juma ‘Makapu’, wakati washambuliaji ni Hussein Javu, Amissi Tambwe, Kpah Sherman, Mrisho Ngasa, Jerry Tegete na Simon Msuva. 
  Yanga SC inahitaji ushindi wa ugenini au sare kuanzia mabao 2-2 kufuatia kulazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Etoile katika mchezo wa kwanza Dar es Salaam wiki iliyopita.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: NIYONZIMA AACHWA YANGA SC SAFARI YA TUNISIA, NGONYANI ‘AFUNGA MKANDA’ ANGANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top