• HABARI MPYA

  Sunday, April 26, 2015

  MKENYA ASHINDA LONDON MARATHON YA 'MAHELA KIBAO'

  MWANARIADHA wa Kenya, Eliud Kipchoge ameshinda 'za mahela kibao' London Marathon akimshinda Mkenya mwenzake, Wilson Kipsang leo.
  Bingwa huyo wa zamani wa mita 5,000, alimpita mshindi mara mbili, Kipsang katika mita 800 za mwisho, wakimuacha maili mbili Mkenya mwenzao, Dennis Kimetto anayeshukilia rekodi ya dunia.
  Mwanaraidha huyo mwenye umri wa miaka 30 aliyeshinda Medali ya Dhahabu ya Paris mwaka 2003, alitumia saa mbili, dakika nne na sekunde 42 kumaliza.
  Eliud Kipchoge crosses the line ahead of fellow Kenyan Wilson Kipsang to win the London Marathon
  Eliud Kipchoge akikatiaha mstari wa kuashiria amemaliza Marathon mbele ya Mkenya mwenzake, Wilson Kipsang katika London Marathon
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MKENYA ASHINDA LONDON MARATHON YA 'MAHELA KIBAO' Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top