• HABARI MPYA

  Thursday, April 30, 2015

  KOCHA WA PACQUIAO ASEMA; "NINA WASIWASI MAYWEATHER ATAINGIA MITINI JUMAMOSI, KAWA MPOLE GHAFLA"

  KOCH bora wa ngumi miaka saba, Freddie Roach amnaye anamuandaa Manny Pacquiao kwa pambano dhidi ya Floyd Mayweather Jumamosi wiki hii amezua hofu kuelekea mchezo huo wa karne.
  Roach ana wasiwasi Mayweather anaweza asitokee ulingoni kutokana na kukuza kwa mgogoro wa glavu. Kambi hizo mbili zinavutana juu ya glavu gani mabondia hao watavaa.
  Mabondia hao usiku wa jana wailikutana ukumbi wa MGM Grand ambao watapigana Jumamosi katika Mkutano na Waandishi wa Habari kulitangaza pambano lao. 
  "Sifahamu kwa nini Floyd amekuwa mpole kwenye pambano hili. Nina wasiwasi kweli anaweza kujitoa usiku huo,"amesema Roach.
  Floyd Mayweather na Manny Pacquiao wakitazamana mbele ya Waandishi wa Habari jana mjini Las Vegas
  Mayweather and Pacquiao with the WBC welterweight belt which contains 3,000 emeralds
  Mayweather na Pacquiao wakiwa na mkanda wa WBC uzito wa Welter ambao una emeralds 3,000

  "Anazungumza polepole sana. Kinyonge. Sifikiri bondia yeyote anaogopa, lakini sifikiri kama alilitaka hili pambano, alilazimishwa kwa pambano ambalo hakulitaka," amesema Roach.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KOCHA WA PACQUIAO ASEMA; "NINA WASIWASI MAYWEATHER ATAINGIA MITINI JUMAMOSI, KAWA MPOLE GHAFLA" Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top