• HABARI MPYA

    Tuesday, April 21, 2015

    TOTO AFRICANS MKUTANO MKUU JUMAPILI NYAMAGANA

    Toto Africans itashiriki tena Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu ujao
    KLABU ya Toto Africans ya Mwanza, inatarajiwa kufanya Mkutano wake Mkuu wa mwaka Jumapili katika shule ya Msingi Nyamagana mjini Mwanza.
    Ofisa Habari wa Toto, Mariam Juma ameiambia BIN ZUBEIRY leo mjini Mwanza kwamba, Mkutano huo utaanza Saa 3:00 Asubuhi na Ajenda zitakuwa ni taarifa ya mapato na matumizi, kuhusu kujaza nafasi za Mwenyekiti na Wajumbe wawili waliojiuzulu na maandalizi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
    Mariam, mtangazaji wa Redio Metro FM mjini Mwanza, amesema kwamba wanachama wote wanatakiwa kufika mapema ili kushiriki Mkutano huo wa ustawi wa klabu yao.
    “Tunaomba wanachama wote wa Toto wafike Mkutanoni, kwani Mkutano huu ndiyo dira ya timu yetu kwa msimu ujao katika Ligi Kuu,”amesema Mariam. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TOTO AFRICANS MKUTANO MKUU JUMAPILI NYAMAGANA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top