• HABARI MPYA

  Tuesday, April 28, 2015

  MADOGO CHELSEA WAWAPIGA BAO KAKA ZAO, WATWAA NDOO YA FA BAADA YA KUIKUNG’UTA MAN CITY 5-2 JUMLA

  TIMU ya vijana ya Chelsea imewatangulia kaka zao kusherehekea ubingwa- baada ya kuifunga mabao 2-1 Manchester City Uwanja wa Stamford Bridge jana na kutwaa ubingwa wa vijana wa Kombe la FA England.
  Chelsea imebeba taji hilo kwa ushindi wa jumla wa 5-2, baada ya awali kuwafunga City 3-1 katika mchezo wa kwanza. Katika Ligi Kuu ya England, Chelsea inaelekea kuivua ubingwa Man City.
  City ndiyo walioanza kupata bao kupitia kwa Kelechi Iheanacho dakika ya tano, kabla ya Isaiah Brown kuwasawazishia The Blues dakika 15 baadaye. 
  Tammy Abraham akafunga bao ake la tatu dhidi ya City katika mechi mbili za Fainali, dakika ya 35 kuwahakikishia taji la Chelsea, ambalo pia walilitwaa mwaka 2012, na wakawa washindi wa pili mwaka 2013. 
  Mmiliki wa Chelsea, bilionea Mrusi, Roman Abramovic alikuwepo uwanjani kuwashuhudia makinda wa The Blues wakiinua ‘ndoo’ ya vijana ya FA na alikuwa mwenye furaha ya kutosha. 
  Kikosi cha Chelsea kilikuwa: Collins, Aina, Tomori, Clarke-Salter, Dasilva, Colkett, Musonda/Ali dk84, Boga/Palmer dk73, Abraham/Sammut dk68, Solanke na Brown.
  Manchester City: Haug, Maffeo, Adarabioyo, Humphreys, Angelino, Bryan, Wood/Garcia dk68, Nemane, Celina, Iheanacho/Buckley dk71 na Barker.
  Chelsea celebrate with the FA Youth Cup trophy after beating Manchester City 2-1 to seal a 5-2 aggregate win in the final
  Wachezaji wa Chelsea wakisherehekea taji la FA baada ya kuifunga Manchester City mabao 2-1 katika fainai ya pili jana

  PICHA ZAIDI NENDA: 

  http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-3057999/Chelsea-2-1-Manchester-City-agg-5-2-Isaiah-Brown-Tammy-Abraham-target-Blues-seal-FA-Youth-Cup-four-years.html#ixzz3YanYL9Gg 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MADOGO CHELSEA WAWAPIGA BAO KAKA ZAO, WATWAA NDOO YA FA BAADA YA KUIKUNG’UTA MAN CITY 5-2 JUMLA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top