• HABARI MPYA

  Alhamisi, Aprili 30, 2015

  NDANDA WATAKIWA KUMLIPA MCHEZAJI SH MILIONI 2.6, VINGINEVYO…

  Na Baraka Kizuguto, DAR ES SALAAM
  KLABU ya Ndanda SC imeamuriwa kumlipa mchezaji Amiri Msumi kiasi cha fedha sh. 2, 600,000. Pia Kamati ilihoji mkataba kutokuwa na kipengele cha mshahara, na kusema ni lazima mkataba uonyeshe Kaiser ambacho mwajiriwa analipwa.
  Kamati pia imeagiza kuwa vilabu vifahamishwe kuwa fedha ya kusaini mkataba hazitakiwi kulipwa kwa mafungu. Tafsiri ya fedha ya kusaini, ni mchezaji kulipwa fedha yote baada ya kusaini, na si kwa mafungu. Pamoja na uamuzi huo, Katibu Mkuu wa Ndanda SC ametakiwa kuwepo kwenye kikao cha Mei 3, 2015.

  Katibu wa Ndanda FC, Edmund Kunyengana (kushoto). Klabu yake imetakiwa kumlipa Amiri Msumi Sh. Milioni 2.6

  Malalamiko mengine yataendelea kusikilizwa na Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji Mei 3, mwaka huu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: NDANDA WATAKIWA KUMLIPA MCHEZAJI SH MILIONI 2.6, VINGINEVYO… Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top