• HABARI MPYA

  Alhamisi, Aprili 30, 2015

  USIMCHUKULIE POA MAYWEATHER, NAYE AMESOTEA MAFANIKIO YAKE

  KWA sasa Floyd Mayweather ni mtu maarufu na tajiri duniani, anayechezea fedha kwa starehe na anasa. Lakini kuelekea pambano lake kubwa dhidi ya Manny Pacquiao, zimevuja picha zake wakati bado wa kawaida.
  Bondia huyo ambaye mfalme wa kurusha makonde akiwa anajiandaa kwa pambano lake 48,  hajawahi kupigwa na amekwishawadunda mabondia wote wakali kama Oscar De La Hoya, Ricky Hatton, Miguel Cotto, Chris Algieri, na Juan Manuel Marquez (mara mbili).
  Mayweather amesota mno ili kuwa 'Money', yaani Mtu Pesa kama anavyojiita sasa. Ni mafanikio ambayo aliyasotea kwa kufanya mazoezi kwa bidii, ili kuwa fiti na kushinda kila pambano kukuza thamani yake. Sasa ndiye mwanamichezo tajiri duniani, ambaye utajiri wake ni dola za Kimarekani Milioni 600.  
  Pound-for-pound king Floyd Mayweather poses in front of a white sheet background on June 11, 1998 in Atlantic City

  Floyd Mayweather anavyoonekanaa wa kawaida katika picha hii  ya Juni 11, mwaka 1998 mjini Atlantic City.

  GONGA HAPA UKAANGALIE PICHA ZAIDI ZA MAYWEATHER KABLA YA KUWA 'MTU PESA'

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: USIMCHUKULIE POA MAYWEATHER, NAYE AMESOTEA MAFANIKIO YAKE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top