• HABARI MPYA

    Tuesday, April 21, 2015

    CHRIS SMALLING AANGUKA MKATABA MPYA MAN UNITED HADI 2019, ARSENAL WATASUBIRI SANA

    BEKI Chris Smalling amesaini Mkataba mpya Manchester United ambao utamuweka Old Trafford hadi mwaka 2019.
    Beki huyo wa kati wa kimataifa wa England mwenye umri wa miaka 25 amekuwa akihusishwa na mpango wa kuhamia Arsenal baada ya kusotea namba mzunguko wa kwanza msimu huu United. Lakini kuimarika kwa Smalling mzunguko wa pili na kupata nafasi ya uhakika katika kikosi cha kwanza chini ya kocha Mholanzi, Louis van Gaal kunampa maisha zaidi Old Trafford.
    "NInafurahi amesaini Mkataba mpya. Chris ameimarika na kuendelea vizuri ndani ya kipindi kifupi nilichokuwa katika klabu na amekuwa mtu muhimu katika kikosi cha kwanza,"amesema Louis Van Gaal.
    Chris Smalling (left) signs his new Manchester United contract alongside club boss Louis van Gaal
    Chris Smalling (kushoto) akisaini Mkataba mpya pembeni ya kocha wa Manchester United, Louis van Gaal (kulia) leo.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: CHRIS SMALLING AANGUKA MKATABA MPYA MAN UNITED HADI 2019, ARSENAL WATASUBIRI SANA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top