• HABARI MPYA

  Monday, April 27, 2015

  PLUIJM AFIKISHA MECHI 45 YANGA SC LEO. AMEFUNGWA SITA, SARE 10

  Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
  KOCHA Mholanzi, Hans van der Pluijm leo ataiongoza Yanga SC katika mechi ya 45 tangu aanze kuifundisha mwaka jana.
  Yanga SC inacheza na Polisi Moro leo katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, mchezo ambao wakishinda watatangaza ubingwa.
  Pluijm ameiongoza Yanga mara 44 kwa awamu mbili, kwanza akirithi mikoba ya Mholanzi mwenzake, Ernie Brandts Januari mwaka jana na baadaye Januari mwaka huu akirithi mikoba ya Mbrazil, Marcio Maximo.
  Hans van der Pluijm leo anaiongoza Yanga SC katika mechji ya 45 tangu aanze kazi Januari mwaka jana

  REKODI KAMILI YA PLUIJM YANGA SC
  Januari – Juni 2014 
  Yanga SC 0-0 KS Flamurtari Vlore (Ziara ya Uturuki)
  Yanga SC 2-2 na Simurq PIK (Ziara ya Uturuki)
  Yanga SC 2-1 Ashanti United (Ligi Kuu Bara)
  Yanga SC 0-0 Coastal Union (Ligi Kuu Bara)
  Yanga SC 1-0 Mbeya City (Ligi Kuu Bara)
  Yanga SC 7-0 Komorozine (Ligi ya Mabingwa)
  Yanga SC 5-2 Komorozine (Ligi ya Mabingwa)
  Yanga SC 7-0 Ruvu Shooting (Ligi Kuu ya Bara)
  Yanga SC 1-0 Al Ahly (Ligi ya Mabingwa)
  Yanga SC 0-1 Al Ahly (Ligi ya Mabingwa. Yanga ilitolewa kwa penalti 4-3)
  Yanga SC 0-0 Mtibwa Sugar  (Ligi Kuu Bara)
  Yanga SC 1-1 Azam FC (Ligi Kuu)
  Yanga SC 2-0 Rhino Rangers (Ligi Kuu)
  Yanga SC 5-0 Prisons (Ligi Kuu)
  Yanga SC 1-2 Mgambo JKT (Ligi Kuu)
  Yanga SC 5-1 JKT Ruvu (Ligi Kuu)
  Yanga SC 2-1 Kagera Sugar (Ligi Kuu)
  Yanga SC 2-1 JKT Oljoro (Ligi Kuu)
  Yanga SC 1-1 Simba SC (Ligi Kuu)
  Tangu Januari 2015; 
  Yanga SC 2-2 Azam FC (Ligi Kuu Bara)
  Yanga SC 4-0 Taifa Jang’ombe (Kombe la Mapinduzi, Zanzibar)
  Yanga SC 4-0 Polisi (Kombe la Mapinduzi, Zanzibar )
  Yanga SC 1-0 Shaba (Kombe la Mapinduzi)
  Yanga SC 0-1 JKU (Robo Fainali Kombe la Mapinduzi)
  Yanga SC 0-0 Ruvu Shooting (Ligi Kuu)
  Yanga SC 1-0 Polisi Moro (Ligi Kuu)
  Yanga SC 0-0 Ndanda FC (Ligi Kuu)
  Yanga SC 1-0 Coastal Union (Ligi Kuu)
  Yanga SC 2-0 Mtibwa Sugar (Ligi Kuu)
  Yanga SC 2-0 BDF XI (Kombe la Shirikisho nyumbani)
  Yanga SC 3-0 Priosns (Ligi Kuu)
  Yanga SC 3-1 Mbeya City (Ligi Kuu)
  Yanga SC 1-2 BDF (Kombe la Shirikisho ugenini)
  Yanga SC 0-1 Simba SC (Ligi Kuu)
  Yanga SC 5-1 Platinum FC (Kombe la Shirikisho)
  Yanga SC 2-1 Kagera Sugar (Ligi Kuu)
  Yanga SC 2-0 Mgambo JKT (Ligi Kuu)
  Yanga SC 3-1 JKT Ruvu (Ligi Kuu)
  Yanga SC 0-1 FC Platinum (Kombe la Shirikisho Zvashavane)
  Yanga SC 8-0 Coastal Union (Ligi Kuu)
  Yanga SC 3-1 Mbeya City (Ligi Kuu)
  Yanga SC 1-1 Etoile du Sahel (Kombe la Shirikisho)
  Yanga SC 3-2 Stand United (Ligi Kuu)
  Yanga SC 5-0 Ruvu Shooting (Ligi Kuu)

  Pluiijm aliondoka Yanga SC Juni mwaka jana baada ya kuiongoza katika mechi 19, akipoteza mbili tu, kufuatia kumaliza Mkataba wake wa miezi sita na akaenda Uarabuni pamoja na aliyekuwa Msaidizi wake, mzalendo Charles Boniface Mkwasa.

  Hata hivyo, baada ya kufukuzwa Maximo na Msaidizi wake, Leonardo Leiva, Yanga iliwarejesha wote Mkwasa na Pluijm na leo wanatimiza mechi 45 jumla kazini.
  Katika mechi 44 hadi sasa, Pluijm ameiwezesha Yanga SC kushinda 28, sare 10 na kufungwa sita.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: PLUIJM AFIKISHA MECHI 45 YANGA SC LEO. AMEFUNGWA SITA, SARE 10 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top