• HABARI MPYA

  Jumapili, Aprili 26, 2015

  BABA AMTAKA MAYWEATHER AACHE NGUMI

  KOCHA Floyd Mayweather Snr amemtaka mwanaye kushinda vizuri pambano dhidi ya Manny Pacquiao wiki ijayo, lakini baada ya hapo atungike glavu zake kabatini moja kwa moja.
  Mayweather Snr, ambaye alikuwa bondia naye enzi za ujana wake, kabla ya kuwa kocha wa mwanawe huyo, amepuuza wanaosema pambano la Mei 2 ukumbi wa MGM Grand Garden Arena litakuwa la kukata na shoka na kusema kwamba Mfilipino 'hatafua dafu' kwa mwanawe.
  "Zama zimefungwa. Imekamilika. Pacquiao amekamilisha. Anahitaji kufungiwa jela, kwa sababu ni wakati wa kumpumzisha. Pacquiao anahitaji kujifungia mwenyewe," amesema Baba Floyd Jr.
  Floyd Mayweather Jnr has been urged to retire after beating Manny Pacquiao, by his dad
  Floyd Mayweather Jnr ametakiwa na baba yake kustaafu baada ya kumpiga Manny Pacquiao

  "Siyo levo ya Floyd. Yeye ni mpinzani tu. ni hivyo tu. Hakuna zaidi, hakuna pungufu,"amesema.
  Mayweather Jnr, atapanda ulingoni akiwa na rekodi ya kupigana mapambano 47 bila kupoteza, kati ya hayo 26 ameshinda kwa Knockout (KO).
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: BABA AMTAKA MAYWEATHER AACHE NGUMI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top