• HABARI MPYA

  Jumamosi, Aprili 25, 2015

  AZAM FC WAIKATA MAINI SIMBA SC, WAIGONGA STAND UNITED 4-0 CHAMAZI

  Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
  AZAM FC wameendelea vizuri na mawindo ya nafasi ya pili katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kufuatia ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Stand United jioni ya leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
  Azam FC kwa ushindi huo inafikisha pointi 45 baada ya kucheza mechi 23, ikiwa nyuma ya Yanga SC yenye pointi 52 za mechi 23 na mbele ya Simba SC yenye pointi 41za mechi 24.  
  Mabao ya mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu jioni ya leoyamefungwa na Gaudence Mwaikimba mawili, Farid Malik na Mganda Brian Majwega.  

  Majwega alifunga dakika ya 14 akiunganisha kwa shuti maridadi krosi ya kiungo hodari Salum Abubakar ‘Sure Boy’.
  Sure Boy tena akapiga krosi nzuri iliyounganishwa nyavuni na Mwaikimba kwa kichwa krosi dakika ya 37.
  Mwaikimba tena, akaifungia Azam FC bao la tatu dakika ya 62 akimalizia mpira uliotemwa na kipa wa Stand, John Mwenda kufuatia krosi ya Sure Boy.
  Farid Malik aliyetokea benchi kipindi cha pili, aliifungia Azam FC bao la nne dakika ya 89, akimalizia kazi nzuri ya Kipre Tchetche aliyetokea benchi pia. 
  KIkosi cha Azam FC kilikuwa: Aishi Manula, Shomary Kapombe, Gardiel Michael, Agrrey Morris, Serge Wawa, Mudathir Yahya/Bryson Raphael dk55, Frank Domayo, Salum Abubakar, Didier Kavumbagu/Kipre Tchetche dk67, Gaudence Mwaikimba/Farid Malik dk84 na Brian Majwega. 
  Standa United: John Mwenda, Revocatus Richard,  Abuu Ubwa/Yassin Mustafa dk, Jisend Mathias, Peter Mutabuzi, Jonh Nganga, Pastory Athanas/Salum Kamana dk73, Hamisi Shengo, Abasalim Chidiebele, Kheri Mohammed na Tola Anthony/Vitalis Mayanga dk46.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: AZAM FC WAIKATA MAINI SIMBA SC, WAIGONGA STAND UNITED 4-0 CHAMAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top