• HABARI MPYA

  Jumatatu, Aprili 27, 2015

  CHICHARITO AMSUTA HENRY, AIPIGIA MBILI REAL IKICHAPA MTU NNE LA LIGA

  NYOTA ya mshambuliaji Javier Hernandez ‘Chicharito’ imeendelea kung’ara baada ya kuifungia mabao mawili Real Madrid ikiibuka na ushindi wa 4-2 dhidi ya wenyeji Cekta Vigo Uwanja wa Balaidos katika mchezo wa La Liga usiku wa kuamkia leo.
  Real sasa inapunguza pengo la idadi ya pointi inazozidiwa na vinara wa La Liga, Barcelona hadi kubaki pointi mbili (81-79), timu zote zikiwa zimecheza mechi 33.
  Wenyeji ndiyo waliokuwa wa kwanza kupata bao dakika ya tisa kupitia kwa Nolito, kabla ya Real kusawazisha kupitia kwa Toni Kroos dakika ya 16 na Chicharito akafunga la pili dakika ya 24.
  Hata hivyo, wenyeji wakasawazisha tena dakika nne baadaye kupiria kwa Mina, kabla ya James Rodriguez dakika ya 43 na Chicharito dakika ya 69 kuifungia Real bao la tatu na la nne.
  Chicharito ndiye aliyeifungia Real bao pekee la ushindi katika Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Atletico Madrid, lakini Nahodha wa zamani wa Arsenal, Thierry Henry akamkandia ‘kinoma’.
  Alisema alishangilia kama ametwaa Kombe la Dunia- na alishangilia bila ya mtu aliyemoa pasi, Ronaldo ambaye ndiye alifanya kazi kubwa. Na Henry ambaye sasa ni mchambuzi wa Sky Sports, akasema Chicharito anayecheza kwa mkopo kutoka Manchester United, hakucheza vizuri na hana uhakika kama atapewa nafasi zaidi kikosini Real. 
  Javier Hernandez scored two more important goals for Real Madrid as they look to keep up with Barcelona in the quest for the La Liga crown
  Javier Hernandez akishangiia baada ya kuifunjgia Real Madrid mabao mawili jana 

  PICHA ZAIDI NENDA: 

  http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-3056582/Celta-Vigo-2-4-Real-Madrid-Javier-Hernandez-scores-twice-Real-come-La-Liga-title-race-alive.html#ixzz3YTfo2e50 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: CHICHARITO AMSUTA HENRY, AIPIGIA MBILI REAL IKICHAPA MTU NNE LA LIGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top