• HABARI MPYA

  Friday, April 24, 2015

  NUSU FAINALI UEFA NDOGO; NAPOLI VS DNIPRO NA FIORENTINA NA WENYE TAJI SEVILLA

  TIMU za Italia, Napoli na Fiorentina zimetenganishwa katika Nusu Fainali ya Europa League maarufu kama UEFA ndogo. 
  Napoli ya kocha wa zamani wa Liverpool, Rafa Benitez itamenyana na Dnipro, wakati Fiorentina itawavaa mabingwa watetezi, Sevilla.
  Sevilla wakifanikiwa kushinda taji hilo na mwaka huu, kutawafanya Waspanyola hao waweke rekodi ya kulitwaa kwa mara ya nne. 
  Mechi za kwanza za Nusu Fainali ya michuano hiyo zitachezwa Mei 7 na marudiano yatakuwa Mei 14, mwaka huu, wakat Fainali itachezwa mjini Warsaw, Mei 27, mwaka huu.The draw for the Europa League semi-finals was made on Friday morning at UEFA's headquarters in Nyon
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NUSU FAINALI UEFA NDOGO; NAPOLI VS DNIPRO NA FIORENTINA NA WENYE TAJI SEVILLA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top