• HABARI MPYA

  Ijumaa, Aprili 24, 2015

  LIVERPOOL YAMTIA 'PINGU NDEFU' JORDAN HENDERSON

  KIUNGO Jordan Henderson amesaini Mkataba mpya na Liverpool, unaomfanya aongezewe mshahara hadi kufika Pauni 100,000 kwa wiki.
  Nyota huyo mwenye umri wa miaka 24 amesaini Mkataba huo jana asubuhi ambao utamfanya awe mali ya Liverpool hadi mwaka 2020. 
  Mkataba wake wa sasa Henderson, ambaye ni Nahodha Msaidizi wa Liverpool ulikuwa umebakiza miezi 12 na kuongezewa Mkataba mrefu kunaongeza matumaini yake ya kuwa Nahodha Mkuu Merseyside mara Steven Gerrard atakapoondoka kikosi cha Brendan Rodgers mwishoni mwa msimu.
  Jordan Henderson is 'over the moon' after signing a new long-term contract with Liverpool 
  Jordan Henderson amesaini Mkataba mpya mrefu Liverpool 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: LIVERPOOL YAMTIA 'PINGU NDEFU' JORDAN HENDERSON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top