• HABARI MPYA

  Saturday, April 25, 2015

  MSUVA ATIMIZA MECHI 100 YANGA MABAO 34

  Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
  WINGA wa Yanga SC, Simon Msuva jana amecheza mechi yake ya 100 Yanga SC tangu ajiunge na timu hiyo mwaka 2012 akitokea Moro United.
  Msuva alifunga mabao mawili Yanga SC ikiibugiza 5-0 Ruvu Shooting katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, mabao mengine yakifungwa na wageni, Kpah Sherman wa Liberia mawili na Amissi Tambwe wa Burundi moja.
  Katika Ligi Kuu msimu huu, Msuva ametimiza mabao 16 na kuzidi kuwaacha washindani wake katika ufungaji bora, Tambwe mwenye mabao 11, Mrundi mwingine Didier Kavumbangu wa Azam FC mwenye mabao 10 sawa na mzalendo, Rashid Mandawa wa Kagera Sugar.  
  Simon Msuva jana amecheza mechi yake ya 100 Yanga SC akifikisha mabao 34
   

  Kwa ujumla Simon Msuva hadi sasa amefunga mabao 34 tangu ajiunge na Yanga SC, hivyo kuendelea kufuata nyayo za Mrisho Ngassa vizuri.
  Ngassa jumla amiechezea Yanga SC mechi 184 na kuifungia mabao 86. Kabla ya kuondoka kwenda Azam FC na baadaye Simba SC, Ngassa aliifungia Yanga SC mabao 57 katika mechi 121 na aliporejea amecheza mechi 63 na kufunga mabao 29 ndani ya misimu miwili. 
  Bao la 34 katika mechi ya 100; Simon Msuva akiifungia Yanga SC bao la tatu katika ushindi wa 5-0 jana dhidi ya Ruvu Shooting
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MSUVA ATIMIZA MECHI 100 YANGA MABAO 34 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top