• HABARI MPYA

  Alhamisi, Aprili 23, 2015

  VAN GAAL AMPATA MRITHI WA KUDUMU WA CARRICK MAN UNITED

  KLABU ya Manchester United imeanza kumsaka mrithi wa muda mrefu wa Michael Carrick, huku Ilkay Gundogan akionekana kuongoza katika kuwania naafasi hiyo.
  Kocha Louis van Gaal amekuwa akibutiwa mno na mchango wa Carrick Old Trafford msimu huu. Kiungo huyo wa kimataifa wa England amekuwa katika kiwango kizuri na tegemeo la klabu hiyo.
  Lakini akiwa ana umri wa miaka 33, Mholanzi huyo anafahamu kiungo huyo anaelekea ukingoni, na wakati mwingi amekuwa akiandamwa na maumivu yanayomuweka nje ya Uwanja. United itamwaga noti ndefu kumsajili mrithi wa Carrick.
  Kiungo wa Dortmund, Gundogan amekuwa akifuatiliwa kwa karibu na United. Van Gaal anaihusudu ligi ya Bundesliga na anaamini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 ana uwezo wa kuvaa viatu vya Carrick kwa muda mrefu.
  Carrick, ambaye hivi karibuni amesaini Mkataba wa miezi 12 zaidi, ataendelea kuwa ndani ya mipango ya Van Gaal kwa msimu ujao - lakini klabu inajipanga kwa maisha bila yeye.
  United boss Louis van Gaal has been impressed with Carrick's contribution to the team
  Kocha wa United, Louis van Gaal amekuwa akivutiwa na mchango wa Carrick katika timuVan Gaal has identified Borussia Dortmund's Ilkay Gundogan as a long-term successor to Carrick
  Van Gaal amemtambulisha kiungo wa Borussia Dortmund, Ilkay Gundogan kama mrithi wa muda mrefu wa Carrick


  Kocha wa Borussia, Jurgen Klopp asingependa kuona kiungo huyo anaondoka katika kikosi cha Dortmund, lakini Mkataba wake wa sasa Gundogan unamalizika mwishoni mwa msimu ujao na hadi sasa hajasaini Mkataba mpya.
  Dortmund iko tayai kumtia pingu mchezaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani, lakini tu itasikiliza ofa ili kuepuka kumuachia bure mwaka 2016. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: VAN GAAL AMPATA MRITHI WA KUDUMU WA CARRICK MAN UNITED Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top