• HABARI MPYA

  Saturday, April 25, 2015

  ‘STRAIKA’ WA CHAN AJA YANGA SC, KILA KITU SAFI

  Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
  MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Zimbabwe Donald Ngoma (pichani kushoto) yuko mbioni kutua Yanga SC.
  Mchezaji huyo wa FC Platinum amekwishamalizana kimazungumzo na uongozi wa Yanga SC na sasa klabu ya Tanzania ipo katika mazungumzo na klabu ya Zimbabwe.
  Yanga SC iliitoa Platinum katika hatua ya 32 Bora Kombe la Shirikisho Afrika, lakini kocha Mholanzi Hans van der Pluijm akavutiwa mno na Ngoma, aliyecheza moja tu ya Zimbabwe baada ya kukosa mechi ya Dar es Salaam kwa sababu alikuwa majeruhi.
  BIN ZUBEIRY inafahamu mazungumzo baina ya Yanga SC na Platinum yamefikia mahali pazuri na kwa kiasi kikubwa kilichobaki ni utekelezaji wa makubaliano.
  Akiwa na umri wa miaka 26, Ngoma ni mchezaji mwenye uwezo na uzoefu mkubwa, kwani amekwishaichezea Zimbabwe hadi kwenye Fainali za Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN).
  Kocha wa Yanga SC, Hans van der Pluijm amevutiwa na Donald Ngoma afanye naye kazi Jangwani

  Januari 2014, kocha Ian Gorowa alimuorodhesha Ngoma katika kikosi cha Zimbabwe ambacho kilimaliza katika nafasi ya nne CHAN baada ya kufungwa na Nigeria 1-0 katika mchezo wa kusaka mshindi wa tatu.
  Wazi Yanga SC kama watafanikiwa kumpata mchezaji huyo mwenye nguvu, kasi na uwezo mkubwa wa kukaa na mpira, watakuwa wameiongezea nguvu safu yao ya ushambuliaji.  
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ‘STRAIKA’ WA CHAN AJA YANGA SC, KILA KITU SAFI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top