• HABARI MPYA

    Monday, April 27, 2015

    LOGARUSIC AFUNGUA KESI YA ‘KUIFILISI’ SIMBA SC, ATAKA ALIPWE MILIONI 100 NA…KWA KUFUKUZWA MSIMBAZI, CHANONGO NAYE…

    Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
    ALIYEKUWA kocha wa Simba SC, Mcroatia Zdravko Logarusic amewasilisha madai ya Sh. Milioni 112 Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) dhidi ya klabu yake hiyo ya zamani.
    Logarusic alifukuzwa Simba SC Agosti mwaka jana kiasi cha mwezi mmoja baada ya kusaini Mkataba mpya na klabu hiyo, baada ya ule wa awali wa majaribio wa miezi sita ulioanza Desemba 2013 kumalizika.
    Na mwalimu huyo ambaye kwa sasa anafundisha AFC Leopard ya Kenya, anataka alipwe dola 6,000 ambazo ni mshahara wake wa mwezi mmoja, Agosti na dola 50,000 kwa kuvunja mkataba.
    Kesi hiyo ilitarajiwa kusikilizwa jana mbele ya Kamati Sheria na Hadhi za Wachezaji chini ya Mwenyekiti Richard Sinamtwa, lakini ikashindikana kutokana na mapungufu kadhaa na sasa itapangiwa siku nyingine. 
    Zdravko Logarusic anataka alipwe Milioni 112 Simba SC na amefikisha kesi TFF

    Upande wa Simba SC uliowakilishwa na Katibu wake, Stephen Ally uliomba uthibitisho kwa mwakilishi wa Logarusic katika kesi hiyo kama kweli ameagizwa na kocha huyo, lakini ukakosekana.
    Wakili wa Loga akaambiwa aende kupata uthibitisho wa kupewa jukumu la kumuwakilisha Mcroatia huyo na baada ya hapo, kesi itaanza kusikilizwa.
    Aidha, kiungo wa Simba SC, Haroun Chanongo anayecheza kwa mkopo Stand United ya Shinyanga naye ameishitaki klabu hiyo. 
    Chanongo anadai wakati anapelekwa kwa mkopo Stand United Novemba mwaka jana, makubaliano yalikuwa ni kila klabu ilipe nusu katika mshahara wake.
    Hata hivyo, Chanongo amesema kwamba tangu anodoke Simba SC hajawahi kupewa nusu mshahara wake, wakati wa Stand anaendelea ‘kukunja’ kama kawaida bila mushkeli.   
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: LOGARUSIC AFUNGUA KESI YA ‘KUIFILISI’ SIMBA SC, ATAKA ALIPWE MILIONI 100 NA…KWA KUFUKUZWA MSIMBAZI, CHANONGO NAYE… Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top