• HABARI MPYA

  Sunday, April 26, 2015

  MAN UNITED YATUNDIKWA 3-0 NA EVERTON

  MANCHESTER United imekiona cha moto, baada ya kukung’utwa mabao 3-0 na Everton Uwanja wa Goodison Park.
  Kipigo hicho kinaifanya United ibaki na pointi zake 65 baada ya kucheza mechi 34 na kubaki nafasi ya nne, nyuma ya Arsenal pointi 66 za mechi 32, Manchester City pointi 67 za mechi 34 na Chelsea pointi 76 za mechi 32.   
  James McCarthy aliifungia bao la kwanza Everton dakika ya tano, kabla ya John Stones kufunga la pili dakika ya 35 na Kevin Mirallas la tatu dakika ya 74.
  Kikosi cha Everton kilikuwa; Howard, Coleman, Stones, Jagielka, Baines, Barry, Lennon, McCarthy, Barkley/Naismith dk88, Osman/Mirallas dk68, Lukaku/Kone dk87.
  Manchester Utd: De Gea, Valencia, Smalling, McNair, Shaw, Blind, Mata/Di Maria dk63, Ander Herrera, Fellaini/Falcao dk46, Young na Rooney/van Persie dk88.
  Louis van Gaal could scarcely believe what he was seeing as his side found themselves well beaten down despite dominating possession
  Kocha wa Manchester United, Louis van Gaal na wasaidizi wake kwenye benchi wakiwa hawaamini kilichotokea leo

  PICHA ZAIDI NENDA:

  http://www.dailymail.co.uk/sport/football/article-3056147/Everton-3-0-Manchester-United-James-McCarthy-John-Stones-Kevin-Mirallas-pile-misery-Louis-van-Gaal-clinical-Toffees-exploit-defensive-weaknesses-Goodison-Park.html#ixzz3YQZQQ5IV 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN UNITED YATUNDIKWA 3-0 NA EVERTON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top