• HABARI MPYA

  Jumatano, Aprili 29, 2015

  LIVERPOOL SASA KUSUKWA UPYA, RODGERS ASEMA ANATAKA WAWILI HATARI KWELI

  KOCHA wa Liverpool, Brendan Rodgers amesema kwamba anakabiliwa na jukumu la kuisuka upya timu hiyo ili kuwa na kikosi kitakachoweza kuingia nne bora ya Ligi Kuu England hatimaye kucheza Ligi ya Mabingwa.
  Matumaini ya Liverpool kwenda Ligi ya Mabingwa yameanza kuyeyuka baada ya kufungwa 1-0 jana na Hull City, kwani sasa timu ya Rodgers inazidiwa pointi saba na wapinzani wao, Manchester United walio nafasi ya nne.
  Baada ya kumuuza Luis Suarez msimu uliopita na kushuhudia aliyekuwa pacha wake, Daniel Sturridge akiwa nje muda mrefu msimu huu sababu ya majeruhi, Rodgers amekiri ubora wa Liverpool umeshuka.
  Brendan Rodgers admitted that Liverpool had failed in their objective to qualify for the Champions League
  Brendan Rodgers amesema anahitaji kuisuka upya Liverpool iweze kucheza tena Ligi ya Mabingwa
  Rodgers can no longer call on the services of Luis Suarez after he moved on to join Barcelona last summer
  Rodgers hapati tena huduma ya Luis Suarez aliyehamia Barcelona msimu huu

  "Kwa mashabiki na wachezaji wakati wote ni vizuri kama utapata aina ya wachezaji ambao hakika watakusaidia, mmoja au wawili labda tunahitaji," amesema Rodgers.
  "Klabu inahangaika sana na wamiliki watatusapoti katika hilo. Kama wapo na watafaa, klabu itafanya kikla kitu kuwapata. Hiyo ndiyo changamoto ya msimu ujao: kujenga timu ambayo itapita kwenye maji,".
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: LIVERPOOL SASA KUSUKWA UPYA, RODGERS ASEMA ANATAKA WAWILI HATARI KWELI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top