• HABARI MPYA

  Sunday, April 26, 2015

  PFA YATAJA 11 BORA ZAIDI LIGI KUU ENGLAND, CHELSEA YAINGIZA SITA

  MSHAMBULIAJI wa Tottenham, Harry Kane - amejiweka katika mazingira mazuri ya kutajwa kuwa Mwanasoka Bora wa Mwaka Chipukizi katika hoteli ya Grosvenor, London baadaye leo.
  Hiyo inafuatia mshambuliaji huyo kuwa Muingereza pekee kuchaguliwa katika safu ya ushambuliaji pamoja na mpachika mabao wa Chelsea, Diego Costa kwenye kikosi bora cha msimu England cha PFA.
  Wachezaji sita wa Chelsea wametajwa katika kikosi hicho bora cha mwaka cha Chama cha Wachezaji wa Kuliowa.
  Vijana wa Jose Mourinho wanaelekea kutwaa taji lao la kwanza tangu mwaka 2010 na kutawala kwao katika Ligi Kuu kumewafanya waingie kwa wingi katika XI bora wa PFA.
  The PFA Premier League Team of the Year for the 2014-15 season was announced on Sunday
  Timu Bora ya Mwaka ya PFA kwa msimu wa Ligi Kuu England wa 2014-2015 baada ya kutajwa leo
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: PFA YATAJA 11 BORA ZAIDI LIGI KUU ENGLAND, CHELSEA YAINGIZA SITA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top